Mwenyekiti
Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Freeman Mbowe
akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
jana. Wanaomfuatia ni wenyeviti wenza wa umoja huo James Mbatia
(katikati) na Profesa Ibrahimu Lipumba. Picha na Edwin Mjwahuzi
“Wakati
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisema kuwa suala la muundo wa serikali
lilitakiwa kupigiwa kura, Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samwel Sitta
anaendelea kuongoza Bunge kama mchakato ni mali yake binafsi. Baadhi ya
viongozi wa chama hicho wanataka mchakato usitishwe, wengine wanataka
uendelee,” alisema.
Mbatia
alisema Ukawa inashangazwa na Rais Kikwete kwa kitendo chake cha
kufanya ziara ya kutembelea ranchi binafsi ya kufugia wanyama ya
aliyekuwa Rais wa Marekani, George Bush wakati nchi ikiwa katika
sintofahamu ya mchakato wa kupata Katiba Mpya huku watu wa kada
mbalimbali wakitaka mchakato usitishwe.
Profesa
Lipumba alisema: “Wapo wanaosema kuwa Ukawa tumegawanyika. Hilo siyo
kweli kwa sababu waliotusaliti na kuhudhuria vikao vya Bunge hata
asilimia tano hawafiki. Zaidi ya asilimia 95 hatujakwenda bungeni,”
alisema.
Alisema
kuwa Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph
Warioba alitenga masuala ya ardhi, maliasili na Serikali za Mitaa ili
yaingizwe katika Katiba ya Tanganyika, hivyo kuyajadili mambo hayo
katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano si sahihi. Mbowe alisema: “Viongozi
wanaiacha nchi ijiendeshe yenyewe. Ni kama ndege ambayo rubani yupo
lakini ameweka ‘auto pilot’, yaani wameiruhusu ndege ijiendeshe
yenyewe.”
CAG achunguze
Kuhusu
suala la ukaguzi wa hesabu, Mbatia alisema katika vikao vya Bunge la
Bajeti, baadhi ya wabunge walihoji zinakopatikana fedha za kuendesha
Bunge la Katiba na kusema kutokana na hali hiyo, ni vyema CAG
akachunguza kwa undani suala hilo.
Hoja
kutaka Bunge hilo lisitishwe inaungwa mkono na makundi mbalimbali
pamoja na baadhi ya wabunge wa CCM, akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM,
Mwigulu Nchemba (Iramba-Magharibi) aliyesema likiendelea bila uhakika wa
kupata akidi ya uamuzi itakuwa ni kupoteza zaidi ya Sh20 bilioni za
walipa kodi na wananchi hawataelewa.
Topics: MATUKIO
Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Soma na Hizi
Matukio yaliyojili katika ulimwengu wa Teknolojioa Mwaka 2016
MWAKA 2016 umefika ukingoni, kwanizimesalia saa chache kabla ya kuingia 2017. Ahsante kwa...Read more »
31Dec2016TCRA imeziagiza kampuni za simu kutenganisha vifurushi
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeziagiza kampuni za simu kuanzisha vifurushi vinavyote...Read more »
02Oct2015Facebook na UN washirikiana kutoa huduma ya bure ya Internet kwa wakimbizi wa Syria
Facebook na UN yashirikiana kutoa huduma ya bure ya Internet katika k...Read more »
01Oct2015Instagram yaweka rekodi mpya kwa kufikisha idadi kubwa ya watumiaji
Instagram yaweka rekodi mpya kwa kufikisha idadi kubwa ya watumiaji milion...Read more »
01Oct2015Umoja wa Ulaya na China kushirikiana katika utafiti wa 5G
Umoja wa Ulaya unasema kuwa ushirikiano huu utaongezea vituo v...Read more »
01Oct2015shule zote za Serikali kufungwa nchini Kenya
Serikali yatoa agizo la kwa shule zote kufuatia mgomo wa walimu...Read more »
20Sep2015

Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Computer ina uwezo wa kufanya mambo ambayo binadamu...
-
CAREER OPPORTUNITY Preventive Maintenance Planner...
-
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala...
-
OFFICE MANAGEMENT SECRETARY Qualifications: ...
-
Kifaa kinachotambulika kwa jina la OralQuick...
-
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi...
-
Ulikuwa umeishika vibaya na ikakuponyoka na kuangukia...
-
Meli kubwa zaidi ya abiria duniani iliyoundwa katika...
Data Boosta
