Tangu kununuliwa na Facebook miaka minne iliyopita, Instagram imekuwa ikivutia watumiaji wengi wanaoongezeka kila uchao.
Kwa sasa Instagram imeweza kufikisha watumiaji milioni 400 ikiwa asilimia 75 ya watumiaji hao wanatoka nchi za nje mbali na Marekani.
Kulingana na maelezo yaliyotolewa na blog rasmi ya Instagram, iliarifiwa kwamba watumiaji wengi wameongezeka kutoka nchi za Brazil, Japan na Indonesia ambapo picha zaidi ya milioni 80 husambazwa kila siku.