Mkurugenzi wa Facebook Mark Zuckerberg, alitoa maelezo katika mkutano wa baraza la UN na kutangaza mpango wao wa kutekeleza mradi huo kwa ushirikiano wa UN.
Mradi huo utawawezesha wakimbizi wa Syria kutumia huduma ya Internet bila ya malipo ambapo gharama zote zitalipwa na kampuni ya Facebook.
Kufuatia mradi huo, kambi zote za wakimbizi wa Syria zinatarajiwa kuwekwa vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya matumizi ya Internet.