Teknolojia ya mawasiliano ya kizazi cha 5 Maarufu kama 5G (fifth generation) huenda ikavumbuliwa kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Hii ni kufuatia mkataba wa ushirikiano katika utafiti wa teknolojia hiyo uliotiwa saini baina ya China na Umoja wa Ulaya.
Kamishna wa Umoja wa Ulaya anayehusika na Uchumi wa Kidijitali na Jamii Gunther Oettinger alisema, "Teknolojia ya 5G ina umuhimu mkubwa hasa tukizingatia kuwa kiwango cha mawasiliano kinatarajiwa kuongezeka. Ushirikiano wa kimataifa unatarajiwa ili kufikia ndoto hii."
Hata hivyo Naibu Rais wa Umoja wa Ulaya Jyrki Katainen aliomba China kuwa na uhaki na uwazi katika sera na shughuli zao za kibiashara.