Kifaa kipya kinachotumika kupima virusi vya UKIMWI chaundwa kwa Matumizi ya Nyumbani
Kifaa kinachotambulika kwa jina la OralQuick kilichoundwa nchini Marekani sasa chaweza kutumika katika kupima virusi vya UKIMWI kwa kuweka katika ufizi wa meno.
Kwa mujibu wa maelezo matokeo ya hali halisi ya mtu yanabainika baada ya dakika 20 baada ya kupima.
Kifaa hicho kina mfano wa umbo la kifaa cha kupima ujauzito .
Mstari mmoja karibu na herufi ya C ina maana ya kutokuwa na virusi vya UKIMWI huku mstari mmoja karibu na herufi T unabainisha kuwa na virusi hivyo.
Kulingana na tovuti ya kampuni hiyo,kifaa hicho cha OralQuick kina asilimia 90 ya uhakika wa matokeo.
Nchini Malawi maafisa wa afya wameanza kutoa mafunzo ya jinsi ya kutumia kifaa hicho.
Kifaa hicho nchini Malawi kinapewa raia bila ya malipo lakini Marekani kinauzwa kwa dola 65.
Takriban raia 8,000 wamefanyiwa vipimo kwa kutumia kifaa hicho.
CHANZO: oraquick.com
MHARIRI: AbdallahMagana.com