MWAKA 2016 umefika ukingoni, kwanizimesalia saa chache kabla ya kuingia 2017. Ahsante kwa wewe ambaye umekuwa
mfuatiliaji wa website ya TeknoTaarifa.
Ni wazi kwamba mwaka huu kuna mambo mengi ambayo yamefanyika,katika ulimwengu wa teknolojia nimekuwekea baadhi amboni ni pamoja na:-
Kuundwa kwa CPU yenye core 1000
Mwaka 2016 watafiti wa tawi la Davis la Chuo Kikuu cha
California wamesanifu CPU iitwayo Kilocore ambayo ni ya kwanza duniani
yenye core elfu moja, na inaweza kufanya kazi nyingi zaidi kwa kutumia
nishati chache. CPU hiyo ina transista milioni 621, inaweza kutekeleza maagizo
trilioni 1.78 kwa sekunde, na imetengenezwa kwa teknolojia ya CMOS yenye
ukubwa wa nanomita 32 ya kampuni ya IBM.
Hasara kwa Samsung Galaxy Note 7
Mwaka huu utasalia kuwa pigo kwa kampuni hii ya Kikorea kwani
tumeshuhudia ikikumbana na wakati mgumu kwenye simu zake za Galaxy Note
7, ambapo Oktoba mwaka huu kampuni hiyo iliamua kuagiza kurejeshwa
sokoni kwa simu hizo zote kufuatia kuwapo kwa malalamiko kila kona ya
dunia kutoka kwa wateja juu ya kulipuka kwa simu hizo.
Kwasasa huwezi kupanda ndege iwapo utakuwa na simu ya Note 7 jambo ambalo limetia doa brand ya kampuni hii.
Kutumika kwa Magari ya umeme Kenya
Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza mwaka huu wa 2016. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo.
Kufa kwa simu za BlackBerry
Pia tumeshuhudia kampuni ya BlackBerry iliyokuwa ikijulikana kwa
kutengeneza simu zinazotumia batani, ikiachana kabisa na utengenezaji wa
simu.
BlackBerry ilitangaza ifikapo Septemba kuwa ingeachana na
utengenezaji simu na kujikita kwenye kuendeleza Software zake, kampuni
hiyo imekuwa na wakati mgumu sokoni kwa kipindi kirefu.
Kabla ya kuja kwa simu za iPhone, simu za kampuni hiyo zilikuwa
zikipendwa zaidi duniani
kufa kwa simu za Motorola
Pia kumeshuhudiwa kampuni ya Lenovo ikiiua ile ya Motorola mapema mwaka huu, badala yake kwasasa kampuni hizo zinajulikana kama “Moto by Lenovo”.
iPhone kuachana na headphone jack
Septemba mwaka huu kwa mara ya kwanza kampuni ya utengenezaji simu za iPhone ya Apple imeachana na headphone zilizozoeleka kutumiwa na kampuni hiyo za ‘jack’ na kutambulisha headphone mpya ambazo hazitumii waya za ‘AirPods’, zilizoenda sambamba na uzinduzi wa simu yake mpya ya iPhone 7.
Licha ya kwamba itachukua muda kwa wateja kuzizoea lakini hiyo ni moja ya kampeni ya Apple ya kuhakikisha kuwa wanawekeza nguvu kubwa kwenye soko la sauti.