Meli kubwa zaidi ya abiria duniani iliyoundwa katika karakana ya Saint-Nazaire kusini mwa Ufaransa, imeanza kufanyiwa majaribio baharini.
Meli hiyo inayotambulika kwa jina la "Harmony of the Seas'', itasafiri baharini kwa siku tatu chini ya ulinzi.
Meli hiyo ambayo ina urefu wa mita 362, upana wa mita 66, na urefu wa mita 70, ina uwezo wa kubeba abiria 8,000.
Meli hiyo yenye uzito wa tani 227,000 pia inasemekana kuwa na madaraja 16 yaliyojengwa ndani yake.
Katika kipindi cha msafara wa majaribio, meli hiyo itahudumiwa na wataalamu zaidi ya 2,000.
Abiria wanaotaka kusafiria meli hiyo, watalazimika kununua tiketi zinazoanzia fedha Euro 400-1,200 kulingana na ubora wa sehemu kukaa.
Meli hiyo ambayo tayari imeshanunuliwa na shirika moja la Marekani, inatarajiwa kuanza rasmi safari za kibiashara tarehe 12 mwezi Mei katika bahari ya Mediterania.
Tazama Picha zaidi za Ndani na Nje ya Meli hiyo
CHANZO: dailymail.co.uk
MHARIRI: Abdallahmagana.com