Faida Za Juice Na Unga Wa Ubuyu
Ubuyu kama tulivyozoea wengine wanauweka rangi na sukari unatengenezwa vizuri tunafanya kula na kuna wengine ule unga wake hutengenezea juice au ice cream lakini huu ubuyu una faida zake nyingi katika mwili wa binadamu.
faida zake ni hizi.
Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo
Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
Huongeza nuru ya macho mtu anauwezo wa kuona vizuri
Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
Kuongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
Virutubisho vingi vya kulinda mwili
Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
Unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.