Header ads

Header ads
» » Teknolojia mpya ya Hyperloop , Safari ya KM 1000 ndani ya Saa moja

The Hyperloop Transportation Technologies design for Elon Musk's Hyperloop. It hopes to produce a technical feasibility study finished in mid-2015.

Hyperloop itakayowezesha usafirishati wa mizigo au watu kwa kasi sana, mfano safari ya Dar hadi Arusha kukamilika ndani ya nusu saa tuu. Mwaka huu teknolojia hiyo itafanyiwa majaribio rasmi. Kampuni inayosimamia mradi wa teknolojia hiyo, 

Hyperloop Technologies tayari imeonesha maandalizi waliyofikia kuhakikisha ndani ya mwaka huu wanajenga mfumo huo wa usafiri huko North Las Vegas, Nevada, kwa kiwango kidogo kwa ajili ya kuwawezesha kufanya majaribio ya teknolojia hiyo. 

Mabomba spesheli kwa ajili ya njia ya Hyperloop yakiwa tayari eneo la wazi huko North Las Vegas 

Kampuni ya Hyperloop Technlogies inampango wa kufikia mwaka 2020 -21 wawe wameshatengeneza mfumo wa usafiri wa kutumia teknolojia ya Hyperloop. Watatumia mfano mdogo wanaoujenga na kukamilisha mwaka huu kama sehemu ya kujifunza zaidi kabla ya kujenga mfumo mkubwa zaidi na wa gharama kubwa. Teknolojia hii ikianza kutumika itawezesha usafirishaji wa watu na mizago kuwa haraka zaidi kuliko chombo chochoto cha usafiri kinachotumika kwa sasa. 


Mchoro unaoonesha jinsi wasafiri watakavyoweza kukaa katika chombo hicho cha usafiri 


Mchoro ukionesha ubebaji wa kontena la mizigo ndani ya Hyperloop 

Ushindani pia umeongezeka baada ya kampuni nyingine kuibuka inayofahamika kwa jina la Hyperloop Transportation Technologies ya Calfornia ambayo imesema ipo katika mipango ya kutengeneza sehemu ya majaribio ya teknolojia hiyo hiyo ndani ya miezi michache inayokuja. Je una maoni gani juu ya maendeleo haya katika teknolojia? Kufahamu zaidi kuhusu teknolojia hii soma makala yetu iliyopita -> HYPERLOOP: 



Fikiria Kusafiri Kutoka Dar hadi Arusha ndani ya Nusu Saa Tuu! Vyanzo: Mitandao ya Engadget, The Verge. Sambaza Makala Hii: Comments Andika Maoni Yako Kupitia mabomba spesheli ya aluminiam yaliyotolewa hewa kabisa (vacuum), chombo spesheli kitaweza kusafiri ndani ya mabomba hayo kwa hadi mwendokasi (speed) wa km 1000 ndani ya lisaa limoja (km 1000/saa).

References and useful resources:  
>>dailymail.
 
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post