Header ads

Header ads
» » » Teknolojia wanayotumia Wanafunzi nchini China kuibia Mitihani

 wakati huku kwetu bado wanafunzi wanaendeleza njia za kizamani na kubuni mbinu mpya za kuibia majibu au kufanya udanganyifu wakati wa mtihani, wanafunzi wa nchini China ndio wanaongoza katika matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kufanya udanganyifu huo.

Kila kipindi cha mitihani walimu na hata baadhi ya shule zinatumia polisi katika kuhaha na kusaidia katika kugundua njia zitumiwazo na wanafunzi hao. Inasemakana ugumu wa mitihani yao pamoja na kuwa na mfumo unafanana wa nchi kama Tanzania wa kwamba mtihani wa mwisho kubeba miaka yote ya mtu aliyotumia shuleni unachangia katika kukuza tabia hii.

Kali zaidi imetokea hivi karibuni baada ya kugundulika ya kuwa vijana wameendelea zaidi kiteknolojia katika kuhakikisha wanafanikiwa katika kuibia kwa kutengeneza miwani ambayo inarekodi na kutuma picha hizo kwa mwingine. Hii ni katika mtihani maarufu zaidi ujulikanao kwa jina la Gaokao ambao unaweza kuufananisha na ule wa kuhitimu kidato cha sita kwa hapa bongo. Ukaguzi wa wanafunzi kuingia eneo la kufanya mitihani katika gaokao imebidi nao uwe wa kiteknolojia ya juu, na hivyo imekuwa kama vile mwanafunzi anapita uwanja wa ndege.
Afisa Usalama akionesha Miwani aliyokamatwa nayo mwanafunzi

 
Hivi ni baadhi ya vitu vilivyowahi kukamatwa kutoka kwa mwanafunzi aliyekuwa anafanya mtihani. Completely high tech stuffs!

>>>Tafadhali Click link zifutazo kuhungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post