Header ads

Header ads
» » » Matukio yaliyojili katika ulimwengu wa Teknolojioa Mwaka 2016


MWAKA 2016 umefika ukingoni, kwanizimesalia  saa chache kabla ya kuingia 2017. Ahsante kwa wewe ambaye umekuwa mfuatiliaji wa website ya TeknoTaarifa.
Ni wazi kwamba mwaka huu kuna mambo mengi ambayo yamefanyika,katika ulimwengu wa teknolojia nimekuwekea baadhi amboni ni pamoja na:-

Kuundwa kwa CPU yenye core 1000

Video editing computer CPU

Mwaka 2016 watafiti wa tawi la Davis la Chuo Kikuu cha California wamesanifu CPU iitwayo Kilocore ambayo ni ya kwanza duniani yenye core elfu moja, na inaweza kufanya kazi nyingi zaidi kwa kutumia nishati chache. CPU hiyo ina transista milioni 621, inaweza kutekeleza maagizo trilioni 1.78 kwa sekunde, na imetengenezwa kwa teknolojia ya CMOS yenye ukubwa wa nanomita 32 ya kampuni ya IBM.

Hasara kwa Samsung Galaxy Note 7 

Samsung, samsung Galaxy Note 7, Galaxy Note 7 ban, galaxy Note 7 airlines ban, samsung galaxy note 7 banned in the us, Note 7 banned on flights, Note 7 flight ban, Samsung galaxy Note 7 recall, Galaxy Note 7 global recall, Galaxy Note 7 catching fire, Note 7 battery issues, technology, technology news
Mwaka huu utasalia kuwa pigo kwa kampuni hii ya Kikorea kwani tumeshuhudia ikikumbana na wakati mgumu kwenye simu zake za Galaxy Note 7, ambapo Oktoba mwaka huu kampuni hiyo iliamua kuagiza kurejeshwa sokoni kwa simu hizo zote kufuatia kuwapo kwa malalamiko kila kona ya dunia kutoka kwa wateja juu ya kulipuka kwa simu hizo.
Kwasasa huwezi kupanda ndege iwapo utakuwa na simu ya Note 7 jambo ambalo limetia doa brand ya kampuni hii.

Kutumika kwa Magari ya umeme Kenya

 Nissan

 Magari yanayotumia nguvu za umeme yameanza kuuzwa nchini Kenya kwa mara ya kwanza  mwaka huu wa 2016. Magari hayo hayatumii mafuta hata kidogo.


Kufa kwa simu za BlackBerry
photo recovery from blackberry smartphones
Pia tumeshuhudia kampuni ya BlackBerry iliyokuwa ikijulikana kwa kutengeneza simu zinazotumia batani, ikiachana kabisa na utengenezaji wa simu.
BlackBerry ilitangaza ifikapo Septemba kuwa ingeachana na utengenezaji simu na kujikita kwenye kuendeleza Software zake, kampuni hiyo imekuwa na wakati mgumu sokoni kwa kipindi kirefu.
Kabla ya kuja kwa simu za iPhone, simu za kampuni hiyo zilikuwa zikipendwa zaidi duniani

kufa kwa simu za Motorola
 
Pia kumeshuhudiwa kampuni ya Lenovo ikiiua ile ya Motorola mapema mwaka huu, badala yake kwasasa kampuni hizo zinajulikana kama “Moto by Lenovo”.

iPhone kuachana na headphone jack
 apple-iphone-7-no-ditch-kill-remove-headphone-jack
Septemba mwaka huu kwa mara ya kwanza kampuni ya utengenezaji simu za iPhone ya Apple imeachana na headphone zilizozoeleka kutumiwa na kampuni hiyo za ‘jack’ na kutambulisha headphone mpya ambazo hazitumii waya za ‘AirPods’, zilizoenda sambamba na uzinduzi wa simu yake mpya ya iPhone 7.
Licha ya kwamba itachukua muda kwa wateja kuzizoea lakini hiyo ni moja ya kampeni ya Apple ya kuhakikisha kuwa wanawekeza nguvu kubwa kwenye soko la sauti.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post