Header ads

Header ads
» » Hizi ndizo Aina tatu Tofauti za WhatsApp Usizozifahamu


WhatsApp imekuwa ni njia kuu ya mawasiliano ya meseji fupi kwa watu wengi tunaotumia simu-janja. Umaarufu wake unazidi kukua siku hadi siku. Hapa utafahamu kuhusu WhatsApp ile ile ila yenye ‘fleva’ tofauti. Hii inawezekana kwa kutumia 

WhatsApp Plus, 
 
OGWhatsApp na OpenWhatsApp. Hizi ni program zilizozuka na hazipatikani kwenye masoko yoyote ya programu za simu ila tu kwenye kurasa kadhaa za mtandao. Zinatengenezwa na madevelopa huru, wasiokuwa na uhusiano wowote na kampuni ya WhatsApp lakini wamejikita kuwapa watumiaji uhuru zaidi. WhatsApp Plus Whatsapp Plus (+) ilivumbuliwa na developa wa kihispania, Rafalete mwaka 2012. Programu hii ni bure kabisa lakini ina mailipo ya kawaida na rasmi ya WhatsApp. Mpaka sasa, malipo hayo yapo tu kwenye baadhi ya maeneo ambayo huduma za malipo ya kidijitali yanafanya kazi (Afrika mashariki bado hatujahusika). 

Mambo yatakayokuvutia utumie Whatsapp hii: 

– Muonekano Tofauti: Nakshi Nakshi ndio jambo kuu kwenye WhatsApp plus. Utaweza kubadilisha muonekano na hisia nzima ya WhatsApp kutoka humo humo WhatsApp+ kwa kushusha staili (‘Themes’) zaidi ya 700 bure kabisa! Themes zitabadilisha muonekano wa maneno, ‘Wall-paper’, maandishi na hata rangi na kufanya Whatsapp yako kuwa tofauti na kijani ya kawaida. Utaweza mambo mengine mengi, hata kubadilisha rangi ya chata ya WhatsApp yenyewe kuwa rangi unayoitaka. 

– ‘Emoji ’, ‘Emoticons,’ Vibonzo, Vikatuni au ‘Smileys’ zaidi: Hatujajua bado vitu hivi vinaitwaje ila hivi vitu vinatumika sana siku hizi kuonesha hisia. WhatsApp+ ina vibonzo vingi zaidi ya WhatsApp ya kawaida. Kuna tatizo moja hata hivyo, hivi vibonzo vitaonekana na wale watu wenye WhatsApp+ tu. Kama unamtumia mtu asiyekuwa na WhatsApp+, vibonzo havitatokea na alama ya kuuliza itatokea mahali pake. Kwa hiyo basi, ukitaka kufurahia chaguzo hii, huna budi kumtaarifu na mwenzako ambaye aitumia WhatsApp+. 

– Tuma Picha, muziki na video kubwa zaidi: WhatsApp ya kawaida inakupa uwezo wa kutuma hadi MB 2 kwa faili moja ila kwa WhatsApp+, utaweza kutuma zaidi hadi MB 50 za faili kwa wakati mmoja. – Ona ‘Status’ chini ya jina la mtu unaeandikiana nae meseji. Hii ni rahisi zaidi ya WhatsApp ya kawaida, ambapo utaiona status kwa kufungua taarifa zake kwenye jina lake. – Ona picha ya mtu pamoja na jina lake kwenye makundi.. 

OGWhatsApp 


OGWhatsApp inakupa uhuru wa kutumia namba mbili kwenye WhatsApp moja. Unaweza kujiuliza kwa nini mtu ataamua kufanya hivyo ila kuna ukweli kwamba kuna watu wenye namba tofauti, labda moja kwa kazi na biashara na nyingine kwa kuongea na ndugu, jamaa na marafiki. Mtu wa aina hii anaweza kuitumia OGWhatsApp kwa manufaa ya wateja wake na watu wake wa karibu kwa wakati mmoja. OGWhatsApp inaweza kutumika bila ya ku-‘root’ simu (Hii ni lugha ya kitaalamu zaidi) na hivyo inaweza kutumika moja-kwa-moja kama program zingine. Mambo mengine unayoweza kufanya na OGWhatsApp: – Chagua rangi ya ‘icon’ ya WhatsApp – ’Copy’ na ‘paste’ status ya mtu mwengine kwako. – Chungulia (‘preview’) picha bila ya kuihifadhi kwenye simu. – Angalia video, ‘online’ , yani bila kuihifadhi kwenye simu. 
 OGWhatsApp itaifungua video kwenye app nyingineya video (haitacheza ndani ya WhatsApp). – Angalia takwimu za meseji za makundi. 

OpenWhatsApp Open 
 

WhatsApp ilitengenezwa na developa Tarek wa Cairo, Misri.Kabla ya kupata jina la OpenWhatsApp, programu hii ilibeba jina la Wazaap na ilitengenezwa kwa ajili ya Nokia N9 amabayo Tarek aliipenda sana kiasi cha kuamua kuitengenezea WhatsApp yake. Aliitengeneaza OpenWhatsApp akiwa na malengo ya kukubalika na kampuni za WhatsApp na Blackberry ila lengo hilo halikutimia na mwishowe, kwa maelezo yake, Blackberry walimbwaga na kuamua kutoiweka kwenye AppWorld. Mpaka sasa developa huyo hana mahusiano mazuri na Blackberry. 

OpenWhatsApp ya Blackberry 10 ina mambo matatu ya kujisifia: 
 – Inatamba kwa kuwa pekee kwa Blackberry 10: Kwa kuwa ilitengenezwa mahsusi kwa ajili ya Blackberry 10, 

OpenWhatsApp inafanya kazi vizuri sana na simu za mfumo huo. Muonekano wake unarandana sana na mfumo wa Blackberry 10 kiasi kwamba unaweza kujisikia kama unatumia meseji ya Blackberry badala ya WhatsApp yenyewe na inajitahidi kusapoti uwezo wa Blackberry 10 vizuri.
 – Zima ‘Last Seen’ kwenye status yako ili mtu asijue mara ya mwisho ulipotumia WhatsApp. – 
 

           Ona picha za ‘profile’ ya rafiki yako iliyopo na zilizopita hapo hapo. 

 WhatsApp zenye ladha tofauti zinakupa uhuru zaidi ila hata hivyo, kwa watu wengi, WhatsApp ya kawaida inatosha kabisa kufanya mawasiliano. Katika kukupa ujuzi zaidi, tunaamini kwamba kuna watu wachache ambao watapenda mambo amabyo ni zaidi ya kawaida na ni wachunguzi zaidi. Kuwa mchunguzi kunaonyesha ujuzi zaidi na huwashangaza ndugu, jamaa na marafiki. 

Pia inaonyesha kwamba wewe uko ‘current’ na mambo yaliyopo kwenye dunia ya teknolojia ya mawasiliano na hiki ni kitu kizuri. Hatahivyo, ilani: Tumia hizi WhatsApp kwa tahadhari! WhatsApp inajulikana sana na watu wa ughaibuni kwa kuwa na historia mbaya ya mambo ya kiusalama tangu mwanzo wake. Madevelopa wa programu hiyo wanajitahidi sana kupambana kuihakikisha kuwa salama na ya kuaminika. Kuna wahalifu wengi sana duniani na hamna uhakika kwamba hizi WhatsApp nyingine ni salama. Hizi WhatsApp siyo rasmi (‘Official’) na ndiyo maana huwezi kuzipata kwenye soko lolote kati ya i-tunes, playstore, Windows, Nokia wala Blackbery. Hivyo basi, unaweza kufanya maamuzi mwenyewe. Haushauriwi kwa watu wengi kutumia programu hizi moja-kwa-moja isipokuwa tu kama unataka kujaribu na huna hofu na usiri wala faragha ya mawasiliano yako. Pia jua kwamba kama kuna lolote litaongezwa kwenye WhatsApp ya kawaida, hautaweza kuipata haraka.

References and useful resources:  
>>www.phonesreview.co.uk
 
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post