Header ads

Header ads
» » Fahamu Njia rahisi ya Kuondoa Pattern au Password Uliyosahau


 Mambo vipi Rafiki yangu? Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaopendelea kuweka Pattern kwenye simu zenu kwa usalama zaidi, Basi msijali na kuwaza saana kuhusu nini cha kufanya inapotokea umesahau Pattern ya simu yako, Kwa Teknolojia ya leo mambo bado yatakuwa vizuri kama kawaida.

Makala hii itakusaidia kuweza kuondoa pattern ama password (nywila) uliyosahau katika simu yako (Android), zipo njia nyingi kutegemea na aina ya simu au toleo la Android ambalo simu yako inatumia.
Kwa kutumia barua pepe yako na password ya akaunti ya Google.
Simu zote ambazo zinatumia Android Kitkat ambayo ni toleo la 4.4 na nyingine zote ambazo ni matoleo ya nyuma ya hili zenyewe ni rahisi pindi unaposahau password yako, katika kundi hili la simu pindi tu unaposahau pattern ama password yako simu yako itakutaka uingize barua pepe na password yako ya Google ambayo ulijiandikishia katika simu hiyo na kisha simu yako itafunguliwa.
Angalizo! njia hiyo itafanya kazi iwapo umewasha data katika simu.
Kwa kutumia Android Device Manager.
Njia hii simu zote ambazo katika zimewezeshwa programu hii, vile vile njia hii itafanikiwa iwapo tu wakati huo intaneti ya simu itakuwa imewashwa. njia hii inaweza sio tu kubadilisha password ya simu kwenda katika password yako mpya ila pia inaweza kusaidia kufuta mafaili yote yaliyo ndani ya simu – hii ni muhimu kama simu imepotea au kuibiwa.


Fuata hatua zifuatazo kufungua simu uliyoifunga.
1. Tembelea google.com/android/devicemanager kupitia katika simu nyingine ama kompyuta
2. Ingia kwa kutumia barua pepe pamoja na password yako uliyotumia kusajilia katika simu iliyojifunga
3. Tafuta na chagua kifaa ambacho unataka kukifungua (maana kama una vifaa zaidi ya kimoja ulivyo visajili katika huduma hii vyote vitaonekana hapa)
4. Chagua Lock na uinigize password ya muda kisha bonyeza Lock tena
5. Baada ya hapo unatakiwa uone meseji ikithibitisha kuwa kufaa chako kimebadilishwa password
6. Wakati huu katika simu utaona sehemu ya kuandika password inatokea hapa jaza ile password yako mpya.
7. Ingiza pasword na uende moja kwa moja kuiondoa pasword hiyo ya simu yako.
Kufungua simu kwa Apps mbali mbali.


Watengenezaji mbali mbali wa simu wanakuwa na application zao binafsi kwaajiri ya kusaidia kufungua simu iliyojifunga na password kusahaulika, siku zijazo tutaiongelea kwa marefu njia hii kwa undani. Kwa ufupi ni kwamba njia hii inafanya kazi kama njia iliyopita tofauti ni chache na zinatokana na ukweli kwamba zinatengenezwa na watu tofauti.
 

                      Screen ikiwa imefungwa kwa pattern (PICHA NA freeproxyserversites.)
 
Kufungua simu kwa kurudisha industrial default settings
Njia hii hufuta kila kitu katika simu na kuifanya iwe na mpangilio ule ule iliokuwanao wakati inatoka kiwandani. Njia hii ni ndiyo kimbilio la mwisho kwa ikiwa kama mtu umesahau pattern na password, njia hii hufuta mipangilio yoote ya simu na hifanya simu iwe kama mpya na kufuta passwords ama patterns zilizo katika simu.


(PICHA NA freeproxyserversites.)

>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTAGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post