Header ads

Header ads
» » Mtoto wa miaka 9 aliyepigwa picha Usiku Akisoma nje ya mgahawa huko Ufilipino anaendelea kupokea msaada


Daniel Cabrera alipigwa picha akiwa nje ya duka maarufu la Mac Donalds amejikunyata kwenye kibao anachokitumia kama meza ya kuwekea vitabu vyake akifanya mabaki ya kazi aliyopewa shuleni.
Cabrera alikuwa akitumia mwangaza wa bango la kutangaza duka la McDonald kama taa yake akidurusu !


 
Mtoto aliyekosha ulimwengu kwa ari yake
Mwanafunzi wa Uuguzi bi Joyce Torrefranca, ndiye aliyeipiga picha hiyo nje ya mkahawa huo McDonald ulioko katika mji wa Cebu nchini Ufilipino na akaichapisha kwenye mtandao wake wa kijamii wa Facebook na ujumbe
''mtoto huyo amenikumbusha niwekee bidii maishani''
''kwangu mimi kama mwanafunzi ,nilipigwa na mshangao kutokana na ari ya mwanafunzi huyu mdogo aliyekuwa amechutama akikamilisha kazi yake ya shuleni bi Torrefranca aliiambia runinga ya ABS-CBN katika mahojiano.
''kwa hakika ilinipatia changamoto kubwa niendeleee kufanya bidii katika kila jambo linalonikabili''
Muda mchache baada ya bi Torrefranca kuchapisha picha hiyo kwenye Facebook maelfu ya watu waliichapisha pia wakisema kuwa ilikuwa imewavutia sana.
Sasa wahisani wamejitokeza kwa wingi kufadhili elimu yake.
Mamake kijana huyo Christina Espinosa anasema kuwa Cabrera anapenda shule na masomo yake licha ya shida chungu nzima wanazokabiliana nazo hususan umaskini.
''ameniambia mara nyingi tu kuwa mama mimi sitaki kuwa maskani'' alisema Espinosa


null
Bi Joyce Torrefranca akihojiwa katika moja ya runinga ya taifa
Aidha Cabrera ambaye nyumba yao haina stima amepewa taa zenye mwangaza wa kutosha na wahisani mbali na dawati la kisawasawa ilikumwezesha kusoma bila bugdha.
Na kwa sababu angependa kuwa afisa wa polisi, maafisa wa polisi katika mji huo wa Cebu walimpeleka katika moja ya maduka maarufu ya wanasesere na kumnunulia moja mfano wa gari la polisi.
Hata hivyo misaada imekuwa mingi kupita matarajio yake na mamake bi Espinosa na sasa kanisa lililoko karibu na kwao limekubali kupokea bidhaa zaidi kwa niaba yao.
Vilevile afisa anayeshughulia maswala ya watoto ameingilia kati na kusema kuwa sasa wameanza kuweka mikakati ya kuhakikisha ufadhili wowote unaomkusudia kijana huyo unamnufaisha

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post