Header ads

Header ads
» » Benki ya kwanza binafsi kutoka China barani Afrika yaanza kutoa huduma Dar es Salaama


Benki ya Biashara ya China yenye uwekezaji binafsi kutoka China imeanza kutoa huduma zake jijini Dar es Salaam, Tanzania, ikiwa ni hatua muhimu ya uwekezaji usio wa serikali ya China kwenye sekta ya fedha katika nchi za Afrika. Je, Benki hiyo ambayo ni ya kwanza ya aina hiyo barani Afrika ilianzishwa katika mazingira gani, itatoa huduma gani za kifedha kwa kampuni na watu waliopo Tanzania na nchi nyingine za Afrika, na inataka kufikia malengo gani katika siku za baadaye? 
Hivi sasa uchumi wa Afrika unakua kwa kasi na biashara kati ya China na nchi za Afrika inaimarika siku hadi siku. Makampuni na wachina wengi wameanza kuwekeza barani Afrika, na mahitaji yao kwa huduma za kifedha pia yanaongezeka na kuwa ya aina mbalimbali. Mkuu wa Benki ya Biashara ya China Yan Gang amesema Benki hiyo ilizaliwa katika mazingira hayo.
"Afrika hakika itakuwa ni eneo jingine litakalochangia zaidi ukuaji wa uchumi wa dunia, biashara kati ya China na Afrika inazidi kuongezeka, mwaka jana thamani ya biashara hiyo ilifikia dola za kimarekani bilioni 200. China na nchi nyingi za Afrika hususan Tanzania pia zina urafiki wa jadi. Kutokana na mambo haya, tunaona huu ni wakati mzuri kwetu kuingia kwenye sekta ya fedha ya Afrika."
Baada ya maandalizi ya miaka miwili na mchakato wa kuidhinishwa na idara za usimamizi wa fedha za Tanzania, hatimaye Benki ya Biashara ya China ilipata leseni na kuanza kutoa rasmi huduma zake nchini humo. Akiwa mkuu wa benki ya kwanza binafsi kutoka China barani Afrika, Bw Yan Gang mwenye uzoefu mkubwa kutokana na kufanya kazi kwa miaka mingi katika benki za nchi zilizoendelea za magharibi anaona Benki hiyo itatoa huduma zake kwa wateja na sekta zinazolengwa.
"Benki yetu hakika itatoa huduma kwa kampuni haswa ndogo na za ukubwa wa kati. Sisi ni Benki ya Biashara ya China, hivyo kwanza tunatarajia kutoa huduma za fedha zinazolenga kushughulikia mahitaji ya kampuni za China zilizopo Tanzania, na pia Tanzania ni soko kubwa, na tutafanya juhudi kadri tuwezavyo kujipanua katika soko la Tanzania."
Katika miaka ya hivi karibuni, uchumi wa Tanzania umekuwa unakua vizuri, sekta ya utalii inaendelezwa kwa kasi, mazingira ya uwekezaji yanaboreshwa na uwekezaji kutoka nje unazidi kuongezeka. Takwimu zinaonesha kuwa kati ya watu milioni 40 wa Tanzania, ni asilimia 17 tu walio na akaunti ya benki. Lakini Bw Yan Gang anaona huduma za fedha na soko la fedha nchini Tanzania vina mustakbali mzuri kutokana na maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo.
"Asilimia ndogo ya watu wenye akaunti ya benki inamaanisha kuwa kuna watu wengi ambao bado hawajanufaika na urahisi unaotokana na huduma za fedha za benki. Lakini watu wengi wataanza kupatiwa huduma za fedha kutokana na maendeleo ya uchumi, hali inayofanana na ilivyokuwa nchini China ilipoanza utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango. Kuhusu soko la ndani ya Tanzania, pia tunatathmini uwezo wetu na kuangalia tunawezaje kujipanua katika soko hilo."
Hivi sasa, kuna mashirika 50 ya kifedha ya aina mbalimbali nchini Tanzania, na ikiwa benki ya kwanza binafsi ya China China barani Afrika ambayo ilichelewa kidogo kuingia Tanzania, Benki ya Biashara ya China inawezaje kukabiliana na ushindani wa soko la fedha, na ina malengo gani? Bw Yan Gang anasema,
"Nguvu yetu ni utaratibu wetu, ambao una unyumbufu mkubwa kwenye msingi wa kanuni na utaratibu wa Benki Kuu ya China. Aidha, uwekezaji wa China nchini Tanzania uko hai, ikiwemo miradi ya kiserikali, tunataka kupata oda kadhaa kutoka kwenye miradi hiyo. Upande mwingine ni soko la ndani ya Tanzania, ingawa kuna benki nyingi za biashara za nchi hiyo, lakini zina ukubwa tofauti. Tunaona benki yetu iko katika kundi la kati, na katika miaka mitano na kumi ijayo, tunatarajia kuingia kwenye kundi la juu."

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post