Header ads

Header ads
» » Hii Ndiyo Idadi ya vijana wenye Virusi vya Ukimwi Jijini Dar


Wakati vijana 40,000 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24, wakibainika kuambukizwa ugonjwa wa Ukimwi jijini Dar es Salaam, viongozi, wabunge  na wafanyabiashara wametajwa kuwa vinara wa kusambaza ugonjwa huo.
Mratibu wa Vijana wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (Tacaids), Grace Kessy akizungumza katika warsha ya siku nne ya wawakilishi wa mashirika ya vijana yanayojihusisha na vita dhidi ya Ukimwi nchini jijini hapa alisema, vijana wasipobadili tabia wataendelea kuwapo hatarini.
Alisema katika taarifa zilizokusanywa mwaka 2011 hadi 2012 ilibainika kuwa, kati ya vijana waliopimwa  40,000 walikuwa na maambukizi Dar es Salaam, wakifuatiwa na vijana 10,000 kutoka mikoa ya  Shinyanga, Kagera na Mbeya.
“Tatizo la maambukizi ya Ukimwi ni kubwa hasa kwa vijana hivyo ni muhimu kuwa na mikakati ya pamoja kudhibiti hali hii,” alisema.
Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema akifungua warsha hiyo alisema, suala la kuendelea kuenea kwa Ukimwi ni la kimaadili kwani sasa wanaoharibu watoto ni watu wenye uwezo, wakiwamo wabunge, wafanyabiashara na viongozi kutokana na umaskini wa vijana.
“Taifa lina tatizo kubwa la kimaadili hivi sasa wazazi wameacha jukumu la kulea watoto na kuachiwa wafanyakazi wa ndani, mitandao ya kijamii na simu za mkononi,” alisema.
Alisema ili Taifa lishinde vita hiyo, ni muhimu mashirika hayo kuongeza jitihada za kulinda maadili katika jamii, kupiga vita umaskini na utumiaji wa pombe ovyo kwa kushirikiana na watungaji wa sera.
Awali, mratibu wa mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mtandao wa Mashirika ya Kupambana na HIV katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki, Jovinniah Mollel alisema, vijana kwa sasa wapo hatarini zaidi katika vita dhidi ya Ukimwi.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post