Header ads

Header ads
» » UKAWA WANAITUMIA ESCROW KAMA FIMBO YA KUICHAPA CCM


Wapinzani wamekusudia kuikwamisha Katiba Inayopendekezwa huku wakielekeza nguvu zao kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu kwa lengo la kukiangusha chama tawala.
Mwaka huu una matukio makuu mawili ambayo yanasubiriwa kwa hamu kubwa na Watanzania wengi ili kuandika historia; upigaji kura wa kukubali au kuikataa Katiba Inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.
Mambo hayo yanasababisha wanasiasa na vyama vyao kuwa katika hekaheka kubwa ili kuhakikisha wanashinda katika matukio hayo kulingana na msimamo wao.
Kumekuwapo na mgawanyiko katika suala la kuikubali au kuikataa katiba hiyo na mvutano mkubwa upo kati ya Serikali kwa maana chama tawala cha CCM na wapinzani chini ya muungano wao wa vyama vitatu, Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi ambavyo vinaunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Silaha kubwa wanayoitumia Ukawa kwa sasa katika kuikabili CCM ni kashfa ya ufisadi ya Akaunti Tegeta Escrow na msimamo kwamba hawaiungi mkono Katiba Inayopendekezwa.
Kutokana na hali hiyo, CUF imefanya mkutano mkubwa wa hadhara kwenye uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara ambako ilitumia silaha hizo katika kushawishi wananchi kuiunga mkono.
Katika mkutano huo, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alimwalika mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe ambaye kamati yake ndiyo ilishughulikia sakata hilo kwa kutumia taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Ulikuwa ni mkutano uliopambwa na shangwe na nderemo za kila aina kutoka kwa wafuasi wa CUF waliojitokeza kuwalaki kwenye Daraja za Mikindani na kufanya maandamano ya zaidi ya magari 30, pikipiki 300 na bajaji 40 na pikipiki huku wananchi wakiwa wamejipanga kwenye mistari barabarani.
Baadhi walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali, zikiwemo zilizokuwa na kibwagizo cha “tunataka fedha zetu za Escrow zirudi... Mtumbwi wa Chenge umetoboka”. Andrew Change ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa Kamati ya Uandishi ya Bunge Maalumu la Katiba.
Mbunge wa Mkanyageni, Habib Mnyaa (CUF) alitumia mkutano huo kuwaomba wananchi wa mkoa huo kupiga kura ya ‘hapana’ kwa Katiba Inayopendekezwa wakati muda utakapofika.
Alisema Chenge na wabunge wenzake wa CCM wametengeneza Katiba inayoendelea kulinda maslahi ya wachache badala ya Watanzania wote.
“Ikiletwa hapa katiba ya Chenge ikataeni. Ikataeni, tupeni kule kwani mkiikubali mtakuwa mnaungana na mafisadi kuhalalisha vitendo vya kifisadi viendelee.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post