Header ads

Header ads
» » KWANINI MWEZI JANUARI BEI ZA VIFAA VYA SHULE ZINAPANDA KIOLELA??

Sasa ongezeko la bei za sare na vifaa vya shule linalofanywa na wafanyabiashara sehemu mbalimbali hapa nchini, limewaweka wazazi njiapanda.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa sehemu mbalimbai hasa kwenye maduka ya vifaa vya ofisini katika sehemu nyingi hapa nchini, bei ya sare za shule za msingi na sekondari, madaftari, vitabu na vifaa vingine zimepanda mara mbili ya bei iliyokuwa mwaka jana.
Na hii imeshakuwa desturi kwa wafanyabiashara wengi unapofika wakati wa kufungua Shule ndipo wanaanza kupandisha bei ya vifaa vya Sule, Sijafahamu ni kwa sababu gani? Kwa mfano  mwaka jana bei ya begi la kubebea madaftari lilikuwa likiuzwa Sh10,000, lakini hivi sasa ni Sh20,000.
jozi ya viatu imepanda mara tatu, kwani mwaka jana ilikuwa ikiuzwa kwa Sh5,000 na sasa wananunua kwa Sh15,000 huku bei ya shati, sketi na kaptula ilikuwa Sh4,500 na sasa wanauziwa kwa Sh6,500 mpaka 7,000. hii ni kwa baadhi ya sehemu hapa nchini.
Lakini baadhi ya wafanyabiashara walisema kupanda kwa bei hizo kunatokana na bei za bidhaa hizo kupandishwa katika maduka ya jumla wanakonunua.
“Jola la kitambaa tulilokuwa tunauziwa kwa Sh70,000 hivi sasa tunauziwa kwa Sh120,000, hii ni tofauti kubwa, kwa hiyo hatuwezi kuuza kwa bei ya zamani, lazima tuendane na ununuzi wa jumla ili tupate faida kidogo,” alisema mfanyabiashara mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.
“Hatupendi kupandisha bei, hata sisi tunazidiwa na hatuwezi kufanya biashara kwa hasara tunaenda na soko, kwa hiyo hata wazazi nao wakubali kwenda na mabadiliko hayo ya bei,” alisema.
Wazazi hao wameiomba Serikali ione namna ya kudhibiti upandaji wa bei hizo.
Lakini kaa ujifahamu kwamba kuna wazazi wana watoto zaidi sita na wote wanahitaji kwenda shule, na ukizingatia kipato chao ni cha kubangaiza, Je wataweza kuhimili bei hizi zinazopanda kiolela ususani mwezi huu wa kwanza, Kwa mwendo huu watoto watapelekwa shule kweli?,
Wazazi wanaiomba Serikali kudhibiti upandishwa holela wa bei za vifaa vya shule msimu huu.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post