Katika maelezo yaliyotolewa mtandaoni kupitia tovuti rasmi ya kilabu hiyo, hatua hiyo iliarifiwa kuchukuliwa baada ya maelewano na makubaliano kufanyika kati ya Ronaldinho na Queretaro.
Kilabu ya Queretaro ilitoa shukrani zake kwa Ronaldinho, kutokana na mchango wake aliotoa tangu mwezi Septemba mwaka jana alipojiunga.
Kwa sasa Ronaldinho mwenye umri wa miaka 35 anafuatiliwa na kilabu ya Antalyaspor inayocheza kwenye ligi kuu ya Spor Toto Super League nchini Uturuki.