Mashindano ya Copa America ya mwaka 2015 yaligeuka na kuwa maonyesho ya picha baada ya mechi kati ya Argentina na Jamaica kukamilika.
Jamaica walishindwa 1 – 0 na Argentina na kulazimika kufunga virago baada ya kushika mkia katika kundi B bila pointi yoyote.
Licha ya huzuni uliotanda miongoni mwa mashabiki wa Jamaica kutokana na kubanduliwa kwenye mashindano hayo, wachezaji wa Jamaica walichukuwa fursa hiyo kupiga picha za selfie na nyota wa Argentina Lionel Messi punde tu refa alipopuliza kipenga cha mwisho.
Ushindi huo dhidi ya Jamaica uliiwezesha Argentina kumaliza katika nafasi ya kwanza kwenye kundi B na kujihakikishia nafasi katika hatua ya robo fainali.