Mambo vipi
Rafiki zangu wasomaji wa Website hii, Siku chache zilizopita niliulizwa swali
na Rafiki yangu toka Chuo cha Mipango- Dodoma.
Swali: Ni Jinsi gani unaweza tengeneza Facebook Page?
Tukiachana na hiyo je ushawahi sikia kuwa unaweza badilisha akaunti yako ya facebook na kuwa page? yaani watu wakaanza kuku ‘Like’ baadala ya kuku ‘Add As A Friend’. Najua unaweza ukawa na maswali mawili hapo juu ya kwanini na ni kwa vipi?.. Ngoja nikujibu YoteKama inavyojulikana Facebook ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo inatikisa dunia kwa sasa. Licha ya hivyo pia Facebook wana vipengele vingi sana na bado wanaendelea kutoa vingine vingi ambavyo vinaifanya Facebook izidi kuwa Juu.
Kwa Nini Ubadilishe Akaunti Yako Ya Facebook Kuwa Page
Kama unatumia ukurasa wako wa facebook
kufanya biashara za mtu au hata kutangaza biashara ya mtu si sahihi ni
unakiuka vigezo na masharti. Biashara zote inabidi zifanyike katika
‘Page’ na sio akaunti za kawaida kama unazotumia. Kwa kifupi huruhusiwi
kutumia ukurasa wako wa facebook kuwasilisha kitu kingine chochote
kisichokuwa kinahusiana na wewe kwa mfano biashara yako.
Kutokana na hayo basii unahitaji Page
ili utangaze na kuendesha biashara yako. Sasa si vizuri kuanza na moja
kabisa. Si unaweza tuu kubadilisha akaunti yako ikawa ndio page yako.
Hii itakurahisishia kwa sababu hata watu waliokuwa marafiki zako watakua
ndio watu wako wa kwanza kwanza kulike page hiyo
Pia kumbuka Facebook inaruhusu akaunti
ya kawaida kumiliki marafiki 5000 tuu lakini ukiwa na page hata
kufikisha bilioni inawezekana. Sasa baada ya kujua sababu twende tukajua
tutafanikisha vipi jambo hili.
Jinsi Ya Kubadilisha Ukurasa Wako Wa Facebook Kuwa Page
Kabla ya kuchukua maamuzi ya kuendelea
ni vyema kujua taarifa gani zitahama kutoka katika ukurasa wako na
kwenda samabamba katika Page yako. — Hapa utajua nini kitabaki na nini
kitapotea —
Nini Kitahama
– Kama nilivyosema awali marafiki zako wote na followers wako watakuwa ndio watu wanao ‘ like’ page yako
– Username Yako ndio itakuwa username ya Page Yako
– Picha ya kwenye profile lako ndio itakua picha ya kwenye Page yako
– Bado utakuwa na mamlaka sawa katika Page zingine ambazo unaziendesha
Nini Hakitohama/Kitafutika
Post zako, Picha na Album zote
hazitakuwa zimehama bali zitafutika hivyo Teknokona inashauri uhifadhi
taarifa zako zote kabla ya kufanya zoezi hili
Pia utapoteza cheo chako katika makundi
yote ambayo yapo chini yako. Hivi tunashauri kuwa kabla ya kufanya zoezi
hili uchague mtu na umeweke awe ndio mwendeshaji wa makundi hayo.
Sasa unaweza kuendelea na kubadilisha akaunti yako ya Facebook kuwa Page kwa kufuata Maelekezo haya.
- >Log in katika ukurasa wako wa facebook
- >Fuata (bofya) Link Hii Kuanza kubadilisha Akaunti yako kuwa Page
- >Chagua Aina ya page unayotaka katika machaguo yaliyojitokeza
- >katika kuchagua aina ya page chagua pia ‘Category’ inayokufaa kisha bofya ‘Get Started’