Nchini Sudan Kusini mara kwa mara imetambulishwa kwa kuwa eneo la vita ,mauaji na ghasia,sasa matumaini yameanza kupnekana baada ya raia wa kawaida katika nchi hiyo kuanzisha programu ya michezo ya simu inayosisitiza amani na umoja baina ya wananchi.
Luan Michael Mayen ni kijana mwenye umri wa miaka 24 aliyeunda programu hiyo mpya ya simu inayotambulika kwa jina la 'Salaam'.
Programu hiyo ambayo ni mchezo wa simu unachezwa na mchezaji kwa kuharibu mabomu yote yaliyotegwa,kabla hayajalipuwa raia wasio na hatia,ikiwa mchezaji ameweza kuharibu mabomu yote,ujumbe wa hongera kwa kuokoa maisha ya watu unatumwa .
Kampuni ya Mayen ina programu maalum ya michezo kwa jina la 'Junub'.
Katika michezo hiyo kuna majina kama 'Wahda' inayomaanisha umoja huku Salaam inamaanisha amani.
Mayen ana lengo la kusambaza michezo hiyo kwa raia 200,000 walioko katika kambi za wakimbizi Uganda baada ya kutoroka wakati wa ghasia nchini Sudan Kusini.