Kampuni ya Samsung kutoka Korea Kusini imetambulisha simu zake mpya za Galaxy J5 na Galaxy J7 zinazotarajiwa kuingizwa China kwanza kwa ajili ya mauzo.
Simu hizo mpya za Samsung Galaxy J5 na Samsung Galaxy J7, zinavutia kwa muundo wake wa teknolojia ya hali ya juu ikiwa ni pamoja na kamera maalum iliyopachikwa kwa ajili ya picha za selfie.
Simu hizo zenye LED Flash na kutumia LTE, pia zitatumia kadiwia mbili na F/1.9 Diaphram.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba simu hizo zitakuwa na 1.5 GB RAM, nafasi ya hifadhi yenye ukubwa wa 16 GB inayoweza kuongezwa.
Simu ya Samsung Galaxy J5 ina skrini ya inchi 5 yenye ubora wa HD, ilhali Samsung Galaxy J7 ina skrini ya inchi 5.5 yenye ubora wa HD pia.
Simu hizo zitakazokuwa na magamba ya rangi nyeupe na dhahabu pia zitaendeshwa kwa mfumo wa Android 5.1 Lollipop.