Hongera kwa kumiliki android smartphone. Ni simu nzuri ambazo zinakuwezesha wewe kuzitumia vyovyote vile utakavyo na zikiwa zimejaaliwa uwezo mkubwa wa kuongeza mambo unayoyahitaji wewe. Karibu Studio.

Kwanza kabisa ningependa kukukumbusha kwamba ili uweze kuinstall apps hizi utahitaji kuwa na Google AppStore (Play Store) katika simu yako. Na umeshajiunga nayo, kama haujajiunga ni rahisi, fungua tu account ya Gmail kisha jiunge na Play Store iliyomo katika android yako.
Kwa wale ambao ndio kwanza umenunua smartphones hizi au ulikua nayo na ungependa kuongeza apps au bado unajiuliza ni apps gani za kuweka katika simu yako, leo tutatizama apps 8 muhimu za kuinstall pindi unaponunua smartphone yako ya android (Mfano; Tecno, Samsung, Huawei).
1. Chrome Beta.

Google Chrome ni browser yenye uwezo mkubwa. Ndiyo browser inayotumiwa zaidi duniani lakini pia ina nguvu na uwezo wa kukuonesha webpages kama zilivyo. Bada
Download hapa Chrome Beta
2. Avast AntiVirus

Avast ndiyo antivirus bora ya bure mwaka 2014. Avast ina version mbili moja ya bure na nyingine ya kulipia lakini hizi zote zimedhihirisha kuwa za msaada sana kwa watumiaji wake.
Download hapa Avast Antivirus
3. Whatsapp

Hii inakuwezesha kuwasiliana na marafiki kwa njia ya meseji, video, audio na hata mafaili mbalimbali. Inatumiwa na watu wengi pia duniani.
Download hapa Whatsapp
4. Instagram

Huu ni mtandao unaowezesha mawasiliano kwa njia ya picha. Picha ni rahisi kujieleza. Unaweza kuunganishwa na watu maarufu duniani.
Download hapa Instagram
5. Ccleaner

Hii ni app bomba sana. Inasafisha simu yako kwa kutoa mafaili ambayo hauyaoni lakini yanachukua nafasi katika simu yako. Pia hufuta registry files mbovu.
Download hapa Ccleaner.
6. Cabinet Beta

Inakupatia muonekano na mpangilio mzuri wa simu yako. Hukuwezesha kushare mafaili kwa urahisi.
Download hapa Cabinet.
7. Piktures

Download hapa Piktures
8. Mailbox

Inakuwezesha kusoma e-mails na kuzijibu pia kiurahisi kwa kupitia android yako. Ni app muhimu hasa kwa matumizi ya kujibu e-mail za marafiki au wateja wako.
Download hapa Mailbox.
BONUS:
9. IFTTT

Inamaanisha "If This Then That". Hii app ni nzuri sana kwa kukurahisishia mambo mbalimbali. Inaonekana ngumu lakini kazi yake inavutia. Inaweza kuunganisha programu nyingine kwa pamoja. Lakini pia unaweza kuiset juu ya shughuli kadhaa. Kwa mfano unaweza kuiset kwamba endapo (If This) ukimpigia mama simu (Then That) then itume meseji kwa baba ikimsalimia pia. Hivyo inakurahisishia kuwasiliana na wazazi wako kwa wakati mmoja. Huo ni mfano tu.
Download hapa IFTT