Michael Owen amewekeza kwenye Website ya Michezo
Lengo la TeknoTaarifa ni kukuletea Taarifa murua za Teknolojia kutoka sehemu mbalimbali,
Huwezi kubisha nikikwambia kuwa, eneo hili la teknolojia limekuwa na faida kubwa iwapo litatumika vema, kwani hata wanamichezo wamenusa fursa hii na kuona kumbe wanaweza kutengeneza mkwanja mrefu kwa kufanya uwekezaji kwenye sekta hii.
Kama wewe ni mpenzi na ufatiriaji wa soka najua unalikumbuka hili jina Michael Owen, kwani ni kati ya yale yaliyowahi kusumbua kwenye ulimwengu huu wa soka, ni kweli kwamba ni mchezaji mstaafu wa Timu ya Taifa ya Uingereza, licha ya kwamba amestaafu soka, lakini Owen aliamua kurudi kivingine, safari hii yuko nyuma ya teknolojia.
Owen aliamua kuanzisha website yake ambayo inatambulika kwa Jina la Sportlobster, tovuti hii inahusisha michezo tofauti takribani 32 na ilianzishwa maalum kwa ajili ya mashabiki wa michezo kutembelea na kujua taarifa, matokeo, video mbalimbali kwenye moja ya michezo iliyoko humo. Pia website hiyo inamuingizia kipato kikubwa zaidi kwani ndiyo biashara aliyowekeza baada ya kustaafu soka,
Mashabiki pia kutoka kote ulimwenguni wanaweza kuchati, kupata fununu na hata kutembelea tovuti nyingine. Tovuti hiyo ilizinduliwa mwaka 2013, inapatikana mtandaoni na kwenye Apps za Androids na iOS ambapo inazaidi ya watembeleaji milioni 1.4, akiwamo Cristian Ronaldo ambaye alihusishwa makusudi kwa ajili ya kuipa soko tovuti hiyo.