Kulingana na maelezo yaliyotolewa na msemaji wa White House, iliarifiwa kwamba Rais wa Marekani Barack Obama atazuru Ethiopia kukutana na viongozi wa AU mwishoni mwa mwezi wa Julai.
Ziara hiyo ya makao makuu ya AU nchini Ethiopia itakuwa ni ya kwanza kutekelezwa na Obama tangu kuingia madarakani kama rais wa Marekani.
Maelezo zaidi yanaarifu kwamba ziara hiyo inalenga kuboresha uchumi na demokrasia, pamoja na kuimarisha usalama katika nchi za Afrika.
Baada ya ziara hiyo, Obama ataelekea nchini Kenya kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa ujasiriamali utakaoanyika jijini Nairobi.