Header ads

Header ads
» » Orodha ya Teknolojia na Vifaa vilivyozinduliwa na Kampuni ya Google Mwaka 2016

Zikiwa zimesalia siku chache kuukamilisha mwaka 2016 na kuhukaribisha mwaka 2017, TeknoTaarifa inakufahamisha Teknolojia na Vifaa vilivyozinduliwa na Kampuni ya Google Mwaka 2016

1. Google Pixel na Pixel XL
Hizi ni simu mpya ambazo zitachukua nafasi ya simu aina ya Nexus 5X na Nexus 6P. Zitakuwa baadhi ya simu za kwanza kabisa kutumia mfumo wa Android usioambatanishwa na teknolojia zingine, yaani Android ya kipekee.
Pixel XL imekuja na screen wa inchi 5.5 na vipimo vya pixeli 1440 x 2560 huku pia ikiwa na uwezo mkubwa zaidi wa kudumisha betri. na prosesa za hali ya juu aina ya Snapdragon 821, RAM ya 4GB, skena za vidole, zinajaa moto haraka pamoja na kuwa na kamera ya 12MP. Bei yake bado haijajulikana.


Unreal And Unity Gaming Engine Will Support Google’s Daydream VR2. Daydream VR headset
Daydream ndio mfumo mpya wa Google wa teknolojia ya VR (Virtual Reality) unaoupa ule wa Samsung Gear VR ushindani wa kikweli. VR ya Google imekuja na shimo la kuweka waya ya kusikilizia video unayotazama kwenye maskio.
Inasemekana kwamba kifaa hiki kitauzwa kwa 'bei ya mkulima' ya Sh7,900 ambayo ni ya chini ikilinganishwa na ile ya Samsung. 


3. Google Home
Google Home vs Amazon EchoKifaa hiki kitakuwa na spika ambayo itadhibitiwa na sauti yako mwenyewe.
Ni teknolojia itakayokuwezesha kucheza muziki kwa kutoa maagizo ya sauti, kuuliza maswali ambayo Google Assistant itayajibu kwa ufasaha kulingana na taarifa zilizoko kwenye Google Search.
Itakuwezesha kudhibiti aplikesheni na vifaa vingine vilivyounganishwa na simu yako ukitumia sauti bila kuiguza hata kidogo simu yako.
 

4.Google Andromeda
Microsoft Continuum
 Hii ni OS mpya ambayo itaunganisha OS za Android na Chrome na kuongeza ubora wa faili na udhibiti wa Chrome kutoka kwa kompyuta hadi kwa simu za Android. Andromeda itatumika kwenye tarakilishi za mezani, vipakatalishi, simu na tableti.


5. Google Wi-Fi
Google To Introduce Free Wifi To The Entire World
Hii ni ruta ambayo itaweza kusambaza mawimbi ya intaneti bila waya kwa umbali zaidi kuliko Wi-Fi za awali. Ina uwezo wa kuunganisha mitandao (networks) mingi kuwa mmoja wenye nguvu zaidi na inaruhusu kutumiwa na watu wengi zaidi hata mtaa mzima.


Chromecast Ultra review6. Chromecast Ultra
Huduma hii itawezesha kutazama video kwa live streaming. za 4K na HDR huku ikiwa na shimo la Ethernet linalowezesha kuwa bora zaidi huduma za kutazama video za mbashara. Itakuwa na kasi mara 1.8 kuliko huduma zilizoko za live streaming.
Chromecast Ultra utaipata kwa Sh7,000 pekee. 
Chanzo: cnet.com, pcadvisor.co.uk na pcmag.com

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post