Header ads

Header ads
» » Ronaldinho arejea nyumbani; ajiunga na Fluminense

 Ronaldinho arejea nyumbani; ajiunga na Fluminense

Mchezaji maarufu wa Brazil, kipenzi cha mashabiki wa kabumbu na mshindi wa taji la Ballon d'Or Ronaldinho arejea Brazil

Ronaldinho ambaye alikuwa amesemekana kuelekea timu ya Antalya Spor ya Uturuki, ameamua kubaki Brazil baada ya kuingia mkataba na timu ya Fluminense.
Fluminense ilitangaza habari hii kupitia mtandao wa kijamii wa twitter ambapo walisambaza picha za Ronaldinho akiwa na jezi nambari kumi ya timu hiyo.
Ronaldinho alisalia bila timu baada ya kuondoka kutoka kilabu cha Queretaro cha Meksiko mwezi uliopita.
Mkongwe huyu wa Brazil anakumbukwa sana kutokana na mchango wake katika timu ya taifa ya Brazil iliyotwaa kombe la dunia mwaka wa 2002 na pia kwa kipindi chake akiwa na Barcelona.
Ronaldinho alianza soka katika timu ya Gremio kabla ya kuchezea PSG, Barcelona na AC Milan.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post