Header ads

Header ads
» » PANYA ROAD 36 WAKAMATWA JIJINI DAR ES SALAAM

Msemaji wa jeshi la Polisi   Advera John Bulimba  - SSP.
Msemaji wa jeshi la Polisi Advera John Bulimba – SSP.
Jeshi la Polisi jijini Dares salaam sasa linawashikilia watuhumiwa 36 kwa mahojiano na uchunguzi  kufuatia  kufanya vurugu siku ya jana   katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Polisi   Advera John Bulimba  – SSP amesema kuwa  taharuki iliyotokea jana tarehe 02 Januari, 2015 katika jiji la Dar es Salaam imewahusisha baadhi ya vijana wanaojiita   Panya road.
Ameongeza kuwa  Chanzo cha taharuki hiyo  ni  kulitokana na kuuawa kwa kijana mmoja ajulikanaye kwa jina la Mohamed Ayub na wananchi tarehe 01/01/2015 katika maeneo ya Tandale kwa Mtogole kwa tuhuma za wizi wakati wa mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya.
Hata hivyo tarehe 02/01/2015 majira ya saa tisa mchana yalifanyika mazishi ya kijana huyo katika makaburi ya Kihatu Kagera Mikoroshini na taarifa zilizokuwa zimelifikia Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam ni kwamba baada ya mazishi hayo vijana wenzake na marehemu walijipanga kufanya fujo ili kulipiza kisasi cha mwenzao kuuawa. Aidha, kabla vurugu hizo hazijafanyika na kwa vile Polisi walishaona dalili ya vurugu hizo, tayari walifanikiwa kuzidhibiti.
Baada ya vurugu hizo kudhibitiwa na Polisi, vijana hao walitawanyika kwa kukimbia katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na kuzua taharuki kubwa kwa wananchi kwamba huenda kila walipokimbilia wanampango wa kuwafanyia fujo raia wema, jambo ambalo wasingeweza kulifanya kwa vile Polisi walikuwa wameimarisha ulinzi katika maeneo yote ya jiji.
Kufuatia hali hiyo , Jeshi la Polisi nchini likiwa linaendelea na msako mkali wa kuwabaini na kuwakamata wote wanaojihusisha na uhalifu huo, ” tunawaomba wananchi watulie, wasiwe na hofu na waendelee na majukumu yao kama kawaida.”Alisema Advera.
Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa vijana wananojihusisha na vikundi hivyo kuacha tabia hiyo mara moja.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post