Header ads

Header ads
» » » VANESSA MDEE NA DIAMOND WAMESHINDA TUZO ZA AFRIMA NCHINI NIGERIA

Diamond Platnumz na Vanessa Mdee wameshinda tuzo nyingine za kimataifa za ‘All Africa Music Awards’ (AFRIMA) zilizotolewa usiku wa December 27 huko Lagos, Nigeria.
Vanessa Afrima
Vanessa a.k.a Vee Money ameshinda kipengele cha ‘Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki’, na kuwashinda Wahu (Kenya), Size 8 (Kenya), Muthoni the Drummer Queen (Kenya), Kaz (Kenya) na Jackie Chandiru (Uganda) ambao pia walikuwa wakiwania.
V money
To God be the Glory, ThankYou soo much for voting – I love you #BestFemaleEastAfrica #Tanzaniaaliandika Vanessa.
Diamond amenyakua tuzo ya ‘Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki’ ambayo ilikuwa ikiwaniwa pia na Dr. Jose Chameleone (Uganda), Kidum (Burundi), Maurice Kirya (Uganda) pamoja na Peter Msechu, featuring Amini (Tanzania).
Vanessa na Diamond wote walikuwa wakishindania vipengele viwili lakini wamefanikiwa kushinda kimoja kila mmoja.
Msechu
Msechu akiwa amebeba tuzo ya Diamond
Peter Msechu ni msanii mwingine wa Tanzania aliyekuwa akishindania tuzo hizo lakini kwa bahati mbaya hakufanikiwa kushinda. kupitia Instagram yake alipost picha akiwa amebeba tuzo ya Diamond ambaye hakuweza kuhudhuria tuzo kutokana kwamba yuko kwenye show Burundi.
“THANKS TO EVRYONE WHO VOTED FOR ME AND MY BOY DIAMOND.. FINALY 2014 AFRIMA AWARDS BEST MALE ARTIST IN EAST AFRICA GOES TO @diamondplatnumz @diamondplatnumz AND I ACCEPTED THE AWARDS ON HIS BEHALF.. CONGRATULATION BRO U MADE IT.. AND AS LONG AS IT COMING HOME ITS FOR US ALL TANZANIANS.. WE CELEBRATE. CONGRATULATION TO @vanessamdee FOR WINNING BEST FEMALE ARTIST IN EAST AFRICA. ITS OUR NIGHT AGAIN.” aliandika Msechu.
Vanessa na Msechu walisafiri hadi Lagos kuhudhuria utolewaji wa tuzo hizo.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post