Header ads

Header ads
» » SIMBA NA YANGA KUTIMUA MAKOCHA KUMEKUWA MCHEZO:: PATRICK PHIRI ATIMULIWA SIMBA


Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri
Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri

Baada ya Yanga sasa ni Simba, Phiri na bechi lake lote wametimuliwa Simba na kesho atapewa barua na haki zake za msingi zitafuatia.
MSERBIA GORAN ambaye alishawahi kuifundisha POLICE ya RWANDA ndiye rasmi kocha wa Simba na atasaini mkataba siku ya jumatano jioni.
Mserbia huyo atasaidiwa na kocha kutoka Rwanda anaitwa JEAN MARIE NTAGAWABILA.

Kocha Patrick Phiri amesema ametaarifiwa kuhusiana na kibarua chake kusitishwa.

Phiri raia wa Zambia amesema ni suala la kawaida kumtokea kocha, hivyo hana kinyongo na uongozi wa klabu hiyo.

"Wamenitaarifu kuhusiana na kuachishwa kazi, hili si jambo jipya, ingawa niliona tungeweza kubadilisha mambo.

"Najua Simba wanataka kufanya vizuri, hivyo siwezi kumlaumu mtu na utaona mwendo wa timu yetu ulivyokuwa," alisema Phiri.

Phiri amesema anasubiri kiasi cha fedha alichokuwa anadai ambacho hakueleza ni kiasi gani, halafu ataanza safari ya kurejea kwao Zambia.

"Nikimalizana nao kuhusiana na malipo yangu, nitajua lini ninakwenda nyumbani," alisema Phiri.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post