Kosa la Facebook kugeuza bendera ya Ufilipino,lilionyesha Nchi ipo Vitani
Juni 12 kila mwaka ni Siku ya Uhuru nchini Ufilipino. Ufilipino ilijitwalia uhuru wake kutoka nchi ya Uhispania mnamo Juni 12, 1898 baada ya zaidi ya miaka 300 ya ukoloni.
Katika kuenzi siku hiyo muhimu, Facebook iliwasalimu wa-Filipino kwa kuonesha bendera ya nchi yao. Hata hivyo, bendera hiyo ilikuwa imegeuzwa, kitendo ambacho kuashiria nchi hiyo iko vitani.
Gazeti la Star nchini humo lilibaini haraka kosa hilo:
Kufuatia kosa hili, watumiaji wa mtandao wa Facebook nchini Ufilipino walicheka ingawa wengi walishukuru Facebook kwa kuwatumia salamu za Siku ya Uhuru.
Hata hivyo, kuna watumiaji wa mtandao wanaoendelea kuikosoa Facebook kwa kuweka bendera ya nchi yao kimakosa.
Hii ni namna sahihi ya kuonesha bendera ya Ufilipino. Katika historia ya nchi hiyo, sehemu nyekundu ilionekana juu ya bluu wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia mwaka 1941 mpaka 1945.
Chanzo: theverge.com