Waziri wa elimu, sayansi na teknolojia mhe: joyce ndalichako ameitaka tume ya sayansi na teknolojia (costech), ofisi ya zanzibar kupanua wigo wa upatikanaji wa teknolojia na kuwafikia vijana wengi zaidi ili waweze kutumia ipasavyo fursa za ajira ziliopo. Aliyasema kuna haja ya kubadili mitizamo ya vijana ya kuacha kusubiri kuajiriwa serikalini na badala yake kuamini kuwa kazi za ujasiriamali zinaweza kuwakomboa katika kuendeleza maisha yao na kuondokana na umasikini. Waziri ndalichako, alisema hayo wakati alipotembelea ofisi ya costech zanzibar na kuzungumza na uongozi wa tume hiyo katika ofisi zake ziliopo maruhubi. Mapema mratibu wa tume hiyo zanzibar dk. Afua mohammed amesema costech zanzibar imeshaanza mpango wa kuwajengea uwezo watendaji wa serikali, ili kuangalia uwezekano wa matumzii ya tafiti kusaidia katika utungaji wa sera. Ameelezea baadhi ya mafanikio yaliopatikana tangu kuanzishwa kwa ofisi hiyo kwa zanzibar, kuwa ni pamoja na upatikanaji na ufaulishaji wa teknolojia, ambapo wakulima wa mazao mbalimbali, ikiwemo mwani wameweza kunufaika