Mabasi ya Abiria yasiyokuwa na dereva yaanza kutumika Paris Ufaransa.
Manispaa ya Paris imeanzisha utumizi wa mabasi yanayotumia umeme kusafirisha abiria kwa masafa mafupi.
Usafirishaji kwa kutumia mabasi hayo unafanyiwa majaribio kwa muda wa miezi 3.
Utumizi wa mabasi hayo ya umeme ni katika juhudi za kupunguza uchafuzi wa anga.
Magari hayo yanasemekana kuwa na kamera maalum, na yanaweza kubeba jumla ya abiria 10.
Aidha magari hayo pia yanaenda mwendo wa pole pole.
Kwa kawaida jijini Paris msongamano wa magari na uchafuzi wa hewa huongezeka zaidi majira ya baridi.
Manispaa ya mji huo ili kupunguza utumizi wa magari ya kibinafsi pia imefanya usafiri wa umma kufanywa bila malipo .