Nabii Samwel Mahela akiwa katika maombezi.
Dotto Mwaibale
MSANII wa Filam aliyejitambulisha kwa
jina moja la Jane amedai amepona ukimwi baada ya kuombewa katika Kanisa
la Pentecostal Power Ministry (PPM) lililopo Mikochezi A.
Akizungumza mbele ya waumini wa kanila
hilo Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii wakati akitoa ushuhuda wa
kupona ugonjwa huo alisema ana mshukuru mwenyezi mungu na Mchungaji
kiongozi wa Kanisa hilo Nabii Samweli Mahela kwa kumuombea na kupona.
"Nampashukurani zangu mungu kwa
kuniponya kupitia mtumishi wake Nabii Mahela nimeteseka sana na ugonjwa
huu aleluya sasa nimepona" alisema Jane na kushangiliwa na waumini wa
kanisa hilo.
Jane alisema alianza kuugua ugonjwa huu
zaidi ya miaka 10 iliyopita na kupata matibabu katika hospitali
mbalimbali bila kupata nafuu mpaka alipoambiwa na mmoja wa waumini wa
kanisa hilo aliyemtaja kwa jina la Onesmo kuwa kuna watu wanapona baada
ya kuombewa katika kanisa hilo na Nabii Mahela.
'Baada ya kuambiwa kuhusu uponyaji huo
nilifika kanisani hapa na kuonana na Nabii Mahela ambaye alinifanyia
maombi mfululizo na kuona hali yangu ikibadilika na sasa afya yangu
imeimarika" alisema Jane.
Akizungumza na Jambo Leo kuhusu suala
hilo Nabii Mahela alisema mbele za mungu hakuna lisilo wezekana kama
ilivyowezekana kwa Jane kwa kuwa aliamini atapona kwa maombi na kweli
amepata nafuu jambo la kumshukuru mungu.
"Biblia inasema kila aaminie atapona kwa jina la kristo na ndivyo ilivyotokea kwa Jane" alisema Nabii Mahela.