Header ads

Header ads
» » Ni Muhimu kuonyesha adabu unapotumia Simu yako ya Mkononi


2 full Google Glass Can Be Used To Steal Your Passcodes
 
Mambo vipi Rafiki zangu wapendwa?. Nikiwa kama Mhariri na Mwandishi wa Habari za Teknolojia Nimewaandalia Makala   inayohusu Adabu katika matumizi ya Simu zetu.
Je kwa mfano Unazungumza ana kwa ana na rafiki yako, na ghafula unapokea ujumbe wa simu. Unapaswa kufanya nini?
  1. Kuusoma ujumbe huo huku ukizungumza na rafiki yako.
  2. Kumwambia rafiki yako “samahani” kisha usome ujumbe huo.
  3. Kupuuza ujumbe huo na kuendelea kuzungumza na rafiki yako.
Kati ya mambo hayo, je, kuna lolote unalopaswa kufanya? Jibu ni ndiyo!

UNACHOPASWA KUJUA

Kumwandikia rafiki yako ujumbe huku ukizungumza na rafiki mwingine ni kama kucheza mchezo uupendao bila kuzingatia sheria za mchezo huo. ‘Lakini hawa ni rafiki zangu,’ huenda ukajitetea. Na hiyo ndiyo sababu unapaswa kuwa na adabu. Si kwamba uwe mtu asiyependa mzaha wala ucheshi. Lakini huu ndio ukweli wa mambo: Usipokuwa na adabu unapokuwa na rafiki zako, baada ya muda wataacha kuwa rafiki zako.
Kwa nini? Kwa sababu watu hawapendi kudharauliwa. Watu wengi huudhika wanapozungumza na rafiki ambaye anatazama simu yake kila mara kana kwamba anatazamia jambo bora zaidi! Unafikiri Watu wa aina hii wataendelea kumvumilia rafiki huyo kwa muda gani?
Ili kuchunguza unavyotenda unapopokea ujumbe wa simu, fikiria hali iliyotajwa kwenye sehemu ya “Kikwazo.” Ungechagua kutumia dokezo gani? Inaelekea, umetambua kwamba Dokezo la A si la adabu. Lakini vipi kuhusu Dokezo la B na C? Je, ni kukosa adabu kukatisha mazungumzo ili usome ujumbe wa simu? Au je, ni utovu wa nidhamu kupuuza ujumbe wa simu ili uendelee na mazungumzo?

UNACHOWEZA KUFANYA

Tuma ujumbe wa simu wakati unaofaa.  
 Sio kila wakati au maali panafaa kutumia simu yako kwa mawasiliano, Laa kuna maali pengine hapastaiki hata kidogo matumizi ya simu, kwa mfano unapokuwa na Mazungumzo yamsingi na mtu au kikundi cha Watu inatakiwa kuiweka simu yako kipya (silent)

Uwe mwenye adabu.  
Mawasiliano yanahusisha maneno, sauti, sura, na mwili wako. Lakini unapoandika ujumbe huwezi kutumia mambo hayo yote. Basi, unawezaje kutumia busara? “Tumia maneno yanayoonyesha adabu, Uliza, ‘Unaendeleaje?’ na utumie maneno kama vile ‘tafadhali’ na ‘asante"

Tumia utambuzi.  
Fikiria tena hali iliyo kwenye sehemu ya “Kikwazo.” Kama unatazamia ujumbe muhimu, huenda ikafaa kuomba radhi na kukatisha mazungumzo. Hata hivyo, huenda si ujumbe wa dharura. Bado utakuwa na simu yako baada ya kumaliza kuzungumza na rafiki yako,  lakini huenda rafiki yako atakuwa ameondoka utakapomaliza kusoma na kujibu ujumbe wa simu. Vivyo hivyo, unaweza kutumia utambuzi unapokuwa katika kikundi. Usitume na kupokea ujumbe muda wote, Kufanya hivyo ni kama kuwaambia watu, Sitaki kushirikiana nanyi, afadhali ningekuwa mahali pengine.

Fikiria kwa makini kabla ya kutuma ujumbe.  
Je, inawezekana kwamba ujumbe wako utaeleweka vibaya? Je, unaweza kuongeza picha ndogo kuonyesha hisia inayofaa? “Kama unafanya mzaha, weka picha ya mtu anayetabasamu,  Huenda watu wakaumia hisia, na hata kukawa na mgogoro, wasipoelewa kwamba ujumbe uliotuma ni wa mzaha.

Jambo la kufikiria: Adabu inategemea upendo. Sifa hiyo huonyeshwaje? Vitabu vya Mungu vinasema “Upendo ni wenye ustahimilivu na wenye fadhili. Upendo hauna wivu, haujigambi, haujivuni, haujiendeshi bila adabu, hautafuti faida zake wenyewe, hauchokozeki.”

  • Picha na Anextweb

>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post