Header ads

Header ads
» » Nchi ya Uganda yatengeneza Basi la Kutumia Umeme wa Jua


     Solar bus uganda
 Sio mamtoni kama tulivyozoea, hii ni kutoka kwa majirani zetu. Huko Uganda wamefanikiwa kutengeneza na kutambulisha rasmi basi la viti 35 linalotembea kwa kutumia nguvu ya umeme jua (Solar energy). Uganda wanazidi kuonesha ni kwa jinsi gani hawaishii kwenye kujifunza tuu kuhusu teknolojia bali wanaenda hatua za mbele zaidi – utengenezaji. 
 Basi hilo limetengenezwa na shirika la Kiira Motors Corporation (KMC), ambalo linapata luzuku kutoka serikali ya Uganda. Hili si gari la kwanza kutengenezwa na shirika hilo, na nia yao kubwa ni kuhakikisha wanapata wateja ili kuwawezesha kutengeneza na kuuza mabasi hayo. Kupitia mabetri mawili ya umeme wa ziada basi hili litaweza kutembea umbali wa kilomita 80 kwa kutumia chaji iliyopo na ata zaidi kutokana na mabetri hayo kuendelea kuchajiwa kupitia ‘solar panels’ zilizowekwa juu ya basi hilo. 
        Solar bus kiira motors
                              Solar Panels zikiwa juu ya basi hilo 
 Wanategemea kufikia mwaka 2018 wataweza kuwa tayari kutengeneza na kuuza mabasi hayo kulingana na oda watakazozipata. Lakini ili kufikia hatua hiyo shirika hilo linaitaji pesa kutoka kwa wawekezaji wengine nje ya luzuku ya serikali ambayo ni kwa ajili ya utafiti zaidi. $58,000 kwa basi moja!!!!!!! 

 Hiyo ndio bei wanayotegemea kuuzia mabasi hayo, hii ni bei ya juu bado ukilinganisha na kati ya $35,000 hadi $50,000 inayoweza kukupatia mabasi mapya kwa sasa yenye kiwango cha viti 35 vya kukaa. Dola 50,000 za kimarekani ni takribani Tsh Milioni 126 | Kes Milioni 5.9 Mmoja wa wahandisi wa shirika hilo, Doreen Orishaba amesema wanaendelea na utengenezaji huku wakisoma hali ya soko ili kuhakikisha ya kwamba hawaishii kutengeneza na kuonesha tuu bali wafanikiwe kiasi cha kuuza mabasi hayo . Na hili linaweza tokea kama hawataweza kutengeneza kwa kiwango bora na huku bei ikiwa chini ukilinganisha na ushindani uliopo sokoni. 

Source: UBC News

>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post