amishna wa kamati ya amani na usalama ya Umoja wa Afrika Smail Chergui amesema, kupunguza silaha za nyuklia kunapaswa kwenda sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuhimiza matumizi ya amani ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.
Chergui amesema hayo jana mjini Addis Ababa, Ethiopia, katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Majaribio ya nyuklia duniani, ambayo pia ni kumbukumbu ya miaka 25 tangu kufungwa kwa kituo cha majaribio ya nyuklia cha Semipalatinsk nchini Kazakhstan.
Chergui amesema, jamii nyingi, hususan barani Afrika, zinanyimwa faida
ya matumizi ya amani ya nyuklia katika maeneo ya hifadhi ya mazingira,
kudhibiti magonjwa, kilimo, na viwanda.