Serikali ya Italia imetangaza kuidai kampuni ya Google kodi ya fedha Euro milioni 200.
Wakati huo huo, serikali ya Italia pia imeishutumu kampuni ya Google kwa madai ya kuficha mapato yake ya fedha Euro milioni 100 kwa lengo la kukwepa kodi.
Msemaji wa Google alitoa maelezo na kusema kwamba kampuni hiyo imeanza kushughulikia masuala ya kodi katika nchi zinazoendesha shughuli zake za kibiashara.
Msemaji huyo aliongezea kusema kuwa wasimamizi wa kampuni ya Google na viongozi wa Italia wanaendelea kujadili suala hilo linalohusu mzozo wa kodi.
Katika siku za hivi karibuni, kampuni ya Google imekuwa ikishutumiwa kwa madai ya kukwepa kodi hasa katika nchi zilizokosa kanuni maalum za kudhibiti mashirika ya kigeni.
Siku kadhaa zilizopita, Google ilikubali kuilipa Uingereza kodi ya ziada ya fedha Euro milioni 185 baada ya kufunguliwa mashtaka na idara ya ushuru nchini humo.
Kwa upande mwingine serikali ya Ufaransa nayo inaarifiwa kuidai kampuni ya Google jumla ya fedha Euro milioni 500 zinazojumuisha kodi za miaka iliyopita.
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM