kwa lugha nyepesi Project Fi ni mtandao
wa simu unaomilikiwa na Google ambao unafanya kazi kwa mtindo tofauti na
mitandao mingine ambayo tumeizowea. Mtandano huu unakupa huduma za simu za
mkononi na huduma za intaneti kwa kutumia mitandao mingine, simu yako itachagua
kutokana na mahali ulipo ni mtandao gani una shika vizuri na kisha kuutumia huo
kupata huduma.
Project
Fi Inavyofanya Kazi
Mtandao huu unatumia simcard
maalumu ambayo inaweza kushika mtandao zaidi ya mmoja( mfano Tigo Voda na
Airtel ) na pia inakuwa na programu maalumu ambayo inasaidia kuweza kuhama
kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kutegemea na upatikanaji wa signal.
Pia Project Fi inatumia mtandao
kukupa huduma za simu ya kiganjani yaani hata ukiwa sehemu hakuna signal za
mtandao wowote ukiunganisha na WiFi ukapata data basi utaweza kupiga simu na
kutuma ujumbe.
Tofauti
ya project Fi mitandao hii ya kawaida.
Mitandao ya kawaida hutumia simcard
ambazo zinauwezo wa kushika mtandao mmoja tuu na matokeo yake ni pamoja na simu
kukosa mtandao pindi unapokuwa maeneo yasiyofikiwa na mtandao wako.
Mitandao ya kawaida kama Smart
Tanzania haitakupa huduma za kupiga na kupokea simu ama kutuma na kupokea sms
kwa kutumia WiFi kitu ambacho mtandao wa Project Fi unakupatia.
Nchi
project Fi Inapopatikana
Mpaka sasa Project Fi inapatikana
katika nchi 120 na ukiwa katika nchi hizi unaweza kuwasiliana na kutuma sms
bila ya kulipa malipo ya ziada kama ilivyozoeleka katika mitandao ya kawaida.
Huduma hii hata hivyo bado ni kwa
ajiri ya wale ambao akaunti zao za Google zimeandikishiwa kutoka Marekani, kwa
sisi ambao tumeziandikishia hapa nchini itabidi zaidi. Pia kwa sasa huduma hiyo
inapatikana kwa watumiaji wa simu ya Motorola Nexus 6 na matoleo mapya lakini
ni malengo ya Google huduma hiyo ipate kusambaa zaidi nje ya hapo.
Yote kwa yote huduma hii
inasubiriwa na watu wengi ambao usafiri mara kwa mara, na pia katika mataifa
kama yetu itakuwa faida kwani kuna baadhi mtandao wako unaweza ukawa na
intaneti isiyo na kasi ukilinganisha na mitandao mingine. Sambaza Makala Hii:
Mazungumzo Andika Maoni Yako Kwa kutumia simu card maalumu ya Project Fi basi
simu yako inaweza kupata huduma zote za simu ya mkononi (kupiga na kupokea
simu, kutuma ujumbe ama huduma za intaneti) kwa kupitia mitandao mingine ambayo
ina miundombinu kama minara na WiFi ambazo zimejiunga na umoja huo chini ya
Google (Google wanaingia mkataba na makampuni hayo ya simu kuiwezesha huduma
hiyo) “ ” Kwa sasa kuna kifurushi cha dola 20 za Marekani (takribani 42,000/=)
mteja anapata dakika, na sms bila kikomo za nchini mwake (kwa sasa Marekani) na
huduma ya sms nchi zote duniani bila kikomo.