Canon imetangaza kuboresha kisimbuzi cha kioo cha kamera kinchoweza kunasa picha katika ubora wa 250 MP.
Kutokana na maboresho hayo, watumiaji wa Canon wataweza kunasa picha za HD katika kipimo cha pikseli 19580 x 12600.
Kisimbuzi hicho cha 250MP kilichokuwa kwenye kioo cha upana wa 9.2 x 20.2mm (APS-H), kwa sasa kinaweza kutumiwa na kamera ya Canon iliyoudnwa kwa ajili ya majaribio pekee.
Kamera hiyo inatoa picha na video zilizokuwa na ubora kwa mara 125 zaidi ya ubora uliopo wa kamera za HD za sasa. Vile vile picha na video zinaweza kunaswa vyema katika umbali wa kilomita 18.