Microsoft iliyobainishwa mpango wake wa kuondoa programu 7, imesema kwamba itaondoa programu 5 kwa sasa, kisha baadaye itaondoa nyingine 2 zilizobaki.
Microsoft inadaiwa kuchukuwa hatua hiyo ili kuboresha muonekano wa picha kwenye mfumo wa Windows.
Miongoni mwa programu zilizoondolewa kwa sasa ni Lumia Storyteller, Lumia Beamer, Photobeamer, Lumia Refocus, Lumia Panorama na Video Uploader.
Hata hivyo baadhi ya programu kama vile Lumia Panorama na Video Uploader, zinaarifiwa kwamba zitaendelea kufanya kazi ingawa hazitofanyiwa usasishaji wala maboresho.