Baada ya uamuzi huo, Orban alimpa Istvan Simicsko mamlaka ya kuongoza Wizara ya Ulinzi.
Simicsko alikuwa akihudumu kama katibu mkuu wa Wizara ya Rasilimali tangu mwaka 2014.
Kwa mujibu wa maelezo ya ofisi ya habari za serikali, inaarifiwa kwamba kabla ya Hende kuwasilisha barua ya kujiuzulu, baraza la usalama la kitaifa lilikuwa limekutana kwa ajili ya kujadili suala la uhamiaji na kupokea ripoti ya ujenzi wa uzio wa kilomita 175 mpakani mwa Hungary na Serbia.
Hende ambaye amekuwa akihudumu kama Waziri wa Ulinzi tangu mwaka 2010, aliwasilisha barua ya kujiuzulu baada ya mkutano huo.