Kuna taarifa kuwa chanzo cha kifo cha ghafla cha rapper Mangweir ni
kuzidisha madawa ya kulevya aliyotumia usiku wa kuamkia leo. Inadaiwa
kuwa Mangwea alikuwa pamoja na mtu aitwaye M TO THE P ambaye naye yupo
mahututi kwa sasa.
Hata hivyo mwenyeji wa rapper Albert Mangwea aliyefariki leo jijini
Johannesburg nchini Afrika Kusini, amesema hit maker huyo wa Mikasi
amefariki akiwa usingizini.
Akiongea na Clouds FM muda mfupi uliopita, mwenyeji huyo aitwaye
Jonathan amesema usiku wa kuamkia leo Mangwair alirudi nyumbani
alikofikia akiwa mzima wa afya lakini mpaka kunakucha hakuonesha dalili
za kuamka.
“Sijui hata huko alitumia nini,” amesema.
Ameongeza kuwa asubuhi kulipokucha aliondoka kuendela na mishemishe
yake na alipokuwa huko wenzake walimpigia simu kumtaarifu kuwa
wamempeleka hospitali ya St. Helen ya jijini humo kwakuwa alikuwa bado
hajaamka na ndipo walipogundua kuwa ameshafariki.
Hata hivyo amesema hakuweza kujua sababu za kifo cha Ngwair kwakuwa
maelezo ya daktari yalikuwa kitaalam kiasi cha kushindwa kuelewa. Ngwair
alikuwa amepanga kurudi leo nchini.
Awali Bongo5 ilizungumza na Bushoke anayeishi jijini Pretoria ambaye
amesema alikuwa akutane naye leo jijini Johannesburg lakini alishangaa
kutompata kwenye simu. Amesema baada ya kuwatafuta washkaji ambao ni
wenyeji wake ndipo walipomuambia kuwa Ngwair amefariki.
“Unajua Ngwair ni mshkaji wangu sana yaani hata siamini kama amefariki aisee,” amesema Bushoke.
Bushoke amesema kesho amepanga kwenda Johannesburg kujionea mwenyewe.
Taarifa za kifo cha Ngwair zimepokelewa kwa mshtuko na watu na
makampuni mbalimbali nchini yametuma salamu za rambi rambi kupitia
kwenye mitandao ya kijamii.
Kilimanjaro Lager
Umeondoka wakati bado tasnia ya muziki inakuhitaji. Pumzika kwa Amani Albert Mangwea “Cowwizy”.
Ndovu Special Malt
R.I.P Albert Mangweir! You will be missed by many Tanzanians.
Adam Nditi
Yani siamini Mangwear amefariki dunia nini ilichomkuta #RIP #Mangwair #akaCowbama
Diva
Jamani Ngwair , am in tears now ….. Jamani!. I can’t believe this. I can’t tweet The RIP….. Whyyyyy?
Home
»
»Unlabelled
» HIKI NDICHO ALICHOKISEMA BUSHOKE AKIWA SOUTH AFRIKA KUHUSU KIFO CHA NGWAIR, SOMA HAPA
Topics:
Imehaririwa na;- poatel Africa
Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
Playstore
TeknoTaarifa Video
TAARIFA ZILIZOSOMWA SANA
-
Kama ni mpenzi wa vitu vikali na bora na umejipanga kuchukua Mzigo mpya wa Kompyuta mpakato “Laptopo” kwa Mwaka huu 2016,Ni...
-
Wana mashabiki wengi, miongoni mwao tayari ni mamilionea (wa shilingi), wapo wenye mijengo, magari ya kifahari, mir...
-
K una watu wengi wenye nguvu katika ulimwengu wa Michezo, Biashara, Siasa,Teknolojia,na mambo mbalimbali, Laki...
-
Mkurugenzi mkuu wa Facebook Mark Zuckerberg amenunua nyumba 4 kwa ajili ya kuzibomoa na kujenga upya katika eneo la Palo Alto lililok...
-
Muonekano wa Kilimanjaro 4 KAMPUNI ya Azam Marine, inaleta boti mpya ya Kilimanjaro 4, ambayo inatarajiwa kuwasili nchini nchini...
-
H atimaye watumiaji wa WhatsApp wataweza kushare nyaraka (Dokoment) kwa Ndugu, Jamaa, Rafiki na wengine zaidi. kipe...
-
Kya GrynDr releases second song of 2013 available for download ! #Wanene Produced by -> @ soundcloud.com/mcivan-thompson Mixed B...
-
Mabingwa wa Bundesliga kufungua kambi ya mazoezi na kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya wahamiaji nchini Ujeruma...
-
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon, amepongeza mafanikio ya kampeni ya kusitisha na kupunguza janga la Ukimwi. Alikuwa akizungum...
Data Boosta