Mchezaji mkongwe wa timu hiyo Robinho aling’aa katika mechi hiyo na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi huo ulioiweka Selecao kileleni.
Nayo timu ya taifa ya Colombia ilijikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimishwa sare tasa dhidi ya timu ya soka ya Peru.
Kwa matokeo hayo, Peru imemaliza katika nafasi ya pili kundi C huku Colombia ikiwa nafasi ya tatu.
Timu zote tatu zimefanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Copa America.
Timu nyingine zilizoungana nazo ni pamoja na Chile, Paraguay, Bolivia, na Argentina.