Timu ya Brazil ilichuana na Serbia kwenye fainali ya kuwania kombe la dunia ilihali wawakilishi kutoka barani Afrika Senegal na Mali, wakatoana jasho kugombania nafasi ya mshindi wa tatu.
Brazil na Serbia zilitoka sare ya 1 – 1 katika muda wa kawaida na kulazimika kucheza katika kipindi cha muda wa ziada ili kuabinisha mshindi.
Hatimaye Serbia walipata goli la ushindi katika muda wa ziada lililofanya mechi hiyo kumalizika 2 – 1 na kubeba ubingwa wa kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia.
Na katika mechi ya mshindi tatu, timu ya Mali ilifanikiwa kumaliza wa tatu baada ya kuicharaza Senegal bao 3 – 1.