Mkali mwingine kutoka afrika akiiwakilisha vyema Nigeria Davido ambae jina lake lilieleweka sana tanzania kutokana na ngoma yake ya "skelewu" lakini pia baada ya kuja kutumbuza kwenye moja kati ya tamasha kubwa tanzania (FIESTA)
Davido ameingia tena kwenye Top story za tanzania tangu Jana June 19 baada ya post yake aliyopost twitter lakini pia na instagram
Davido kwenye post yake Jana alipost Tu bendera ya tanzania bila kuweka caption (maelezo) yoyote zaidi ya kialama cha upendo (love) "♥"
Hii imekua top story kwa tanzania kwa kuwa kwa sasa kuna kinyang'anyiro cha tuzo za MTV Mama ambapo kuna baadhi ya vipengele yuko na mtanzania Diamond platnumz
Siku za hivi karibuni kumekuwa na tuhuma kwamba kuna baadhi ya watanzania si wazalendo wanaendesha kampeni za kumpigia kura Davido wa Nigeria na kumshusha mtanzania Diamond platnumz
Tuhuma nyingi zimezidi zikimwangukia aliyekuwa Mpenzi wa Diamond platnumz na miss tanzania 2006 Wema sepetu hii pia ni baada ya kuonekana kwa comment yake kwenye post ya davido akiwa hajaandika kitu zaidi ya kialama ambacho kinamaana ya furaha kama inavyoonekana kwenye picha
Asante kwa kuisoma hii ....kwa habari nyingine nyingi baki hapa hapa ufahamu mengi
.....Ahsante....