Header ads

Header ads
» » Je kuna atharii za Urais wa Trump katika sekta ya teknolojia na mawasiliano?

  Kwa taarifa yake mtendaji mkuu wa kampuni ya Oracle, Safra Catz ambaye pia alihudhuria kikao cha mazungumzo kati ya Rais mteule wa Marekani Donald Trump na wataalam wa teknolojia ya mawasiliano
alisema, kama Trump ataweza kufanyia kazi mabadiliko kanuni ya kodi, kupunguza udhibiti na kujadili mipango bora ya biashara, teknolojia nchini Marekani itakuwa imara na ya ushindani zaidi kuliko ilivyowahi kutokea awali.
Makampuni maarufu ya kiteknolojia kama vile Apple, facebook na Tesla Motors yalipata nafasi ya kutangaza vipaumbele vyao kama vile mfumo wa kubadilisha taarifa kwenda katika kanuni maalum ambayo itadhibiti kupatikana kwa taarifa kwa mtu ambaye hajaruhusiwa na pia ulinzi wa maudhui ya watumiaji wake.
 Trump Holds Summit With Technology Industry Leaders
Athari za Urais wa Trump katika sekta ya teknolojia na mawasiliano ni ngumu kutabilika, wakati huo kukiwa na uwezekano wa sekta hiyo kupinga mipaka yoyote ya kibiashara pamoja na ukomo wa wahamiaji. Makampuni mengi yanatarajiwa kuunga mkono masuala kadhaa kama vile kupunguzwa kwa viwango vya kodi kwa makampuni hasa katika faida ambayo inapatikana kutoka nje ya nchi.
Kwa upande mwingine, kuna uwezekano wa kuwepo kwa mvutano kati ya Trump na sekta hiyo katika suala la kuthibiti wa upatikanaji wa taarifa ya ujumbe wa siri unaotumwa kupitia katika mitandao, na uwezo wa maafisa wa usalama na idara za ujasusi kuweza kutumia taarifa hizo kwa kutumia vifaa maalum kubaini ujumbe  na kuendesha uchunguzi katika masuala ya usalama wa kitaifa.
POLITICS-US-TRUMP
Trump kwa upande wake alisema, uongozi wake utakuwa ukifanya kazi kwa kushirikiana na sekta binafsi ili kuboresha mazingira ya kibiashara na kufanya kuwa ya kuvutia kwa makampuni ili kutengeneza nafasi mpya za kazi nchini Marekani.

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post