Header ads

Header ads
» » Fahamu Kama Barua pepe (E-mail) Yako Imesomwa Katika Gmail



Barua pepe (E-mail) ni njia nzuri sana ya kuwasiliana na inatumika sana katika kuwasiliana kibiashara. Ni vigumu sana kujua kama barua pepe yako imesomwa kama usipopata majibu ya aina yeyote kwa yule uliemtumia. Kama ulikua unaisubiria kwa hamu barua pepe kutoka upande wa pili alafu ukaona haiji lazima utakuwa na maswali mengi ya kujiuliza sio? Hilo sio tatizo tena kwani TeknoKona inakuja na maujanja mengine leo juu ya namna ya kujua kuwa email yako imesomwa au bado. Hii ina faida kwako kwa mara nyingine baada ya kukaa na kusubiria E-mail ya mtu unaweza endelea kufanya mambo mengine 

Jinsi Ya Kuona Kama Barua Pepe Imesomwa 
  •  Kwanza kabisa itabidi uongeze Extension ya MailTrack katika kivinjari chako cha Google chrome. Extension hiyo inaweza patikana kwa :- 
  • Nenda kwenye Settings za kivinjari chako cha chrome kisha chagua Extensions. Chini kabisa ya Extension zote ambazo zitajitokeza kwa chini yake kabisa kumeandikwa ‘Get More Extensions’ Bofya hapo. 
  • Ukurasa mwingine ukitokea chagua MailTrack na kisha bonyeza Enter 
  • Ukishafanya hivyo MailTrack itatokea kwa upande wa kulia, bofya Add to Chrome Extension Ya MailTrack 
 
Ukishamaliza kuiweka katika kiivinjari chako, unaweza ukai ‘click’ MailTrack na baada ya hapo Window mpya itafunguka na kukuomba uingize Barua pepe yako. Hapo ndio inapokubidi uingize barua pepe yako ya Gmail. Kumbuka barua pepe hii uyoiingiza lazima iwe ile ambayo unataka kuona meseji kama zitakuwa zinasomwa au laa Kinachofuata itabidi uchague kifurushi unachotaka (kuna vifurushi viwili kila cha kulipia na kile cha bure) kwa sasa chagua cha bure tuu lakini hakitakuwa na vipengele vingi kama vile kile cha kulipia. 

 see when email is read in gmail

Aina Mbili Za Vifurushi Kile Cha Bure Na Cha Kulipia Ukishamaliza zoezi la kuchagua kifurushi, hapo unakuwa umemalizana na zoezi zima na utaweza kujua ni email zipi zimesomwa katika barua pepe zako za gmail kwa kutumia MailTrack. MUHIMU: Barua pepe yako ikisomwa utajua kwani katika eneo lako la sent utaona barua pepe hiyo ikiwa imepigwa tiki mbili (kama zile za WhatsApp) kuonyesha kuwa imeshasomwa 
 track sent email in gmail
Alama Ya Tiki Ikionyesha Email Imesomwa 
Pia utapata Notification katika sehemu ya Desktop katika kompyuta yako 
 email read receipts in gmail
Notification Katika Desktop Fuatilia kwa undani ili kujua kama barua pepe zako ulizotuma katika Gmail kama zimesomwa kwa kutumia ujanja huu (MailTrack) tuliokupa leo. Je unaona hii ni sawa kujua kama barua pepe imesomwa katika Gmail au laa? tupe mawazo yako sehemu ya comment hapo chini.TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia

Source;; techuntold 
>>Lengo langu ni kuakikisha upitwi na Habari za Teknolojia ungana Nami FACEBOOK , TWITTER na INSTGRAM

Imehaririwa na;- poatel Africa

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post