Header ads

Header ads
» » Wanamazingira wazitaka serikali za Afrika kutumia Teknolojia ya nishati endelevu


Wanamazingira barani Afrika wamezitaka serikali za nchi za Afrika kuwekeza zaidi kwenye miradi ya teknolojia ya nishati endelevu, ili kuhakikisha bara la Afrika linakuwa na siku za baadaye zenye neema na zisizo na uchafuzi.
Wakiongea mjini Nairobi kwenye kongamano la ngazi ya juu kuhusu sera, wanamazingira wamezitaka nchi za Afrika kuweka sera na hatua za motisha ili kuhimiza uwekezaji kwenye nishati endelevu.
 
Katibu mkuu wa jumuiya ya haki kwenye masuala ya hali ya hewa mjini Nairobi Bw. Mithika Mwenda, alisema kuhama kutoka kwenye matumizi ya nishati ya visukuku kwenda kwenye matumizi ya nishati endelevu, ni muhimu kwa Afrika kukabiliana na changamoto za kimazingira na kiuchumi.
Bw. Mwenda ametoa mfano wa Kenya ambayo imevutia uwekezaji kwenye nishati ya joto la ardhini na upepo, kutokana na uwepo wa hatua za kutia motisha na uchumi tulivu.

Imehaririwa na;- Unknown

Habari yako! Endelea kutembelea Tovuti ya TeknoTaarifa kwa Taarifa murwa za Teknolojia kutoka ndani na nje ya Tanzania, Tupo kwa ajili ya wapenzi wa Teknolojia.
«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post